ASKOFU MAMA RWAKATARE AZIKWA KANISANI KWAKE MIKOCHENI B, DAR ES SALAAM, LEO
Baadhi ya Waombolezaji wachache wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Morogoro Askofu Mama Getrude Rwakatare yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es Salaam, leo
MIKOCHENI, Dar es Salaam
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Morogoro na Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assembly of God (Mlima wa Moto), Askofu Mama Getrude Rwakatare amezikwa leo katika Kanisa lake hilo lililopo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na waombolezaji wachache wakiwemo wawakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya ndungu kuepuka msongamano kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona
Askofu Rwakatare amefariki dunia Jumatatu wiki hii.
Post a Comment