Haya yanakuja wakati ambapo idadi ya vifo Marekani inaelekea kufikia watu elfu kumi.
Virusi vya corona vimeuathiri karibu ulimwengu mzima na kuwapelekea karibu nusu ya watu duniani kusalia majumbani na kupelekea vifo vya karibu watu sabini elfu.
Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza, hapo jana alitoa hotuba yake ya nne ya dharura katika uongozi wake wa miaka 68 ambapo aliwataka Waingereza na nchi za Jumuiya ya Madola kusalia kuwa kitu kimoja.
Ila kulikuwa na sababu ya kutabasamu katika baadhi ya sehemu Ulaya kwani Italia iliripoti visa vichache zaidi vya vifo katika kipindi cha wiki mbili na Uhispania ikashuhudia visa vyake vya waliofariki vikishuka kwa siku ya tatu mfululizo nayo Ufaransa ikiwa na idadi ndogo ya waliokufa katika kipindi cha wiki moja.
Post a Comment