Idadi ya watu walioambukizwa nchini Kenya sasa imefikia jumla ya watu 158 huku vifo vikiwa ni 6. Kulingana na rais Kenyatta watu 4277 wamefanyiwa vipimo vya virusi vya corona.
Bwana Kenyatta pia amewaagiza Wakenya wote kuvaa barakoa katika maeneo yote ya umma, na kuepuka maeneo yenye mikusanyiko ya watu ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.
Marufuku ya kusafiri mjini Nairobi inaanza rasmi Jumatatu saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki, huku marufuku hiyo Kaunti za pwani, Kilifi, Kwale na Mombasa ikianza za Jumatano wiki hii ikitarajiwa kudumu kwa muda wa siku 21.
Hatua ya kuwekwa marufuku katika kaunti hizo nne imetokana na kaunti hizo kuwa na 96% ya visa vya virusi vya Corona nchini Kenya.
Marufuku hiyo imewekwa dhidi ya safari zote za majini, ardhini na nchi kavu ili kuzuwia maambukizi ya corona yanayoongezeka kwa kasi nchini Kenya na maeneo mengine duniani.
Marufuku hii imetangazwa na rais Kenyatta huku Wakenya wakiendelea kutekeleza amri ya kutotoka nje kuanzia saa moja za jioni hadi saa kumi na moja asubuhi iliyotangazwa wiki iliyopita.
Rais Kenyatta amesema huku janga na corona likiendelea kuikumba Kenya na mataifa mengine duniani, Wakenya wanapaswa kubadili tabia kwa kunawa mikono na kutosogeleana.
Post a Comment