Featured

    Featured Posts

MKAZI WA BUNJU KIZIMBANI AKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI


Na Karama Kenyunko globu ya jamii 

MFANYABIASHARA Msiniege Mwakatumbula (56), Mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili likiwemo la kukutwa akifanya biashara ya madini isivyo halali  mali Serikali na utakatishaji wa fedha.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa  serikali Mwandamizi Wankyo Simon imedai kuwa, Machi Mosi, 2020 huko katika eneo la Bunju B lililopo ndani ya Wilaya ya Kinondoni ijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mwakatumbula alikutwa akifanya biashara ya madini isivyo halali ambayo  ni aina ya Rubi, Corundum, Hessonite, Sapphirenuts, Moonstones, Garnet na Beryl. Yenye uzito A gramu 6451. 80.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo imeelezwa kuwa madini hayo yana thamaninya USD 2,950.73 ambayo ni sawa na Sh. 6,791,518.20 mali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali. 

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa siku na mahali hapo mshtakiwa h uyo alijihusisha na biashara ya madini hayo mali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kujipatia kiasi hicho wakati akijua ama alitakiwa kujua kuwa madini hayo ni zao la kosa tangulizi la kosa la uchimbaji wa madini bila kufuata sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama  hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

 Kwa mujibu wa upande wa Mashtaka,  upelelezi katika kesi hiyo uko katika hatua za mwisho. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 4 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa, mshtakiwa amerudishwa rumande.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana