Featured

    Featured Posts

UTAFITI WA MASHINE YA KUSAIDIA KUPUMULIA KWA WAGONJWA WA COVID 19 WAENDELEA NA TANALEC



Mwenyekiti wa Mtaa wa Levolosi Seif Abdi akipokea vifaa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mwenyekiti wa Madereva stand ya Daladala Kilombero vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona huku akifuatiliwa na Meneja msaidizi wa Tanalec Michael Mangowi Leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
 Sehemu ya msaada uliotolewa na Tanelec Ltd ikiwemo Ndoo 100 za maji Tiririka na Sabuni katoni 100 ikiwa ni kwa ajili ya Mapambano dhidi Ugonjwa wa Covid 19 leo jijini Arusha.
Vifaa vilivyotolewa leo na Tanelec Ltd kwa Serikali ya mkoa wa Arusha ikiwa ni kusaidia kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Sehemu ya wadau walioshiriki hafla hiyo leo iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini

Ahmed Mahmoud Arusha
Tanelec imeanza kufanya utafiti wa mashine za kusaidia wagonjwa kupumulia kwa mashine katika kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 na magonjwa mengine.

Akiongea Meneja msaidizi wa Tanalec Michael Mangowi kwenye hafla fupi ya makabidhiano kwa serikali mkoa wa Arusha ya vifaa vya kutakasa mikono ambazo ni sabuni 100 sanjari na ndoo 100 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Covid 19.

Alibainisha kuwa taasisi hiyo kupitia wafanyakazi wake imeendelea na utafiti wa kutengeneza mashine hizo pamoja na mashine nyengine ya kupita na kumwagiwa dawa ya kutakasa mwili mzima kwa lengo la kuendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa covid 19.

“Tumejipanga kuhakikisha tunaendelea na utafiti wa kuhakikisha tunapambana na ugonjwa wa Covid 19 kusaidia vitakasa mikono na mwili ili kuweza kuisaidia serikali yetu dhidi ya janga la ugonjwa wa covid 19”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alishukuru kwa msaada huo kwa kuwa ugonjwa huo hauchagui viongozi wala mtu yoyote

Alisisistiza kuwa Mkoa wa Arusha umejidhatiti katika kuimarisha udhibiti wa wahamiaji haramu wanaoingia maeneo ya mipaka haswa mpaka wa Namanga uliopo Wilayani Longido pamoja na mpaka wa Ngorongoro uliopo wilayani Ngororongoro unaopakana na nchi jirani ya Kenya

Alisisitiza kuwa kunabaadhi ya watu wameshakamatwa kuhusiana na kupita katika mipaka kwa njia za kinyemela na kuziomba taasisi ,mashirika na watu mbalimbali kujitokeza kwaajili ya kuchangia vitu mbalimbali ili kudhibiti ugonjwa huu wa Corona.

Naye mmoja kati ya wanufaika na msaada huo wa kujikinga na Corona ,Mwenyekiti wa Stendi Kuu ya Mabasi Maulid Rajabu alishukuru kwa msaada huo na kusisitiza kuwa hivi sasa wanajitahidi kutoa elimu juu ya ugonjwa huo sambamba na kuhakikisha kila basi linakuwa na ndoo pamoja na sabuni kwaajili ya kunawia mikono.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana