Featured

    Featured Posts

MKUU OFISI YA RAIS BUHARI AFARIKI DUNIA

Kiongozi wa ofisi ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amefariki baada ya kupatikana na virusi vya Corona.
Kupitia taarifa, ofisi ya Buhari imesema imesikitishwa na kifo cha Abba Kyari ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika utawala wa Rais huyo.Taarifa hiyo imesema kuwa marehemu alifariki jana Ijumaa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Kyari aliyekuwa katika miaka ya sabini, ni mtu wa kwanza mwenye cheo cha juu nchini Nigeria kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, imethibitisha visa 493 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 17.

Haijabainika wazi iwapo Rais Buhari amefanyiwa vipimo vya iwapo ameambukizwa virusi vya Corona, lakini mara kwa mara amekuwa akitoa hotuba akisisitiza kuwekwa vizuizi ili kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana