Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya mtu huyo hakuonesha dalili zozote za Covid-19.
Hatua ya Uganda kuwarudisha makwao raia wa kigeni waliopatikana na ugonjwa wa corona imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi hiyo.
Siku ya Alhamisi waziri wa Afya Ruth Jane Aceng alisema kuwa mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika Mashariki yalikubaliana kila raia wa nchi hizo atakayepatika na na virusi vya ugonjwa wa corona atarjeshwa nyumbani kwa matibabu
Alisema kuwa Uganda kila siku huwapokea hadi madereva 3,000 wa malori kutoka mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na kwamba nchi hiyo haita weza kuwapa huduma za matibabu.
Hapo jana Aprili 17 Uganda ilithibitisha kuwa na mgonjwa mmoja wa corona baada ya kufanyia uchunguzi sampuli 774 miongoni mwa sampuli kutoka kwa madereza wa maroli katika vituo vya mpakani kabla waingie nchini humo.
Sampuli 376 kati ya sampuli 774 zilizopimwa hazikupatikana kuwa na virusi vya corona.
Mapema wiki hii Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliongeza marufuku ya kutotoka nje kwa siku 21 zaida ana kusema kuwa hatua zote zilizotangazwa ilipotangazwa marufuku ya awali zitaendelea kama kawaida.
Hatua hizo ni pamoja na kuzuia kabisa mikusanyiko ya watu. Nyumba za ibada na taasisi zote za elimu zitaendelea kufungwa.
Watu pekee watakaoruhusiwa kutoka na kuendelea na shughuli zao ni wafanyakazi katika sekta muhimu kama afya, ulinzi na usalama, wafanyakazi wa benki na wanahabari.
Post a Comment