Aliyekuwa Mkuu wa uhamiaji Mkoa Wa Kagera Pendo Buteghe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kagera alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa kaimu mkuu wa uhamiaji Kagera Thomas Fush marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.
Fush amesema kuwa kufuatia msiba huo mwongozo wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na makao makuu ya uhamiaji umesubiriwa ili kujua taratibu za msiba na maziko
Post a Comment