Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza siku nyingine 21 kuanzia kesho April 15 hadi April May 05,2020 za Watu kuendelea kubaki nyumbani na kutofanya shughuli ambazo zilipigwa marufuku hapo awali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.
Mpaka sasa watu 54 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na kati yao wanne wamepona. Hakuna kifo kilichoripotiwa kufikia sasa.
Machi 31, Museveni alitangaza marufuku ya watu kutokutoka nje kwa siku 14, ambazo zilikuwa zinaisha leo Aprili 14.
Hii leo, Museveni amesema bado wanahitaji muda zaidi wa kupambana na virusi hivyo na watu waendelee kusalia majumbani mwao.
“Kwakuwa tumeongeza siku 21 za kubaki nyumbani, tutaendelea kugawa chakula kwa makundi mawili, wale ambao walikuwa wanategemea pato la siku kuendesha maisha na wale ambao hawawezi kujitafutia chakula (walemavu, Wazee nk), wenye mishahara kila mwezi hii misaada haiwahusu”- Amesema Museven
Post a Comment