Featured

    Featured Posts

RAIS WA NIGERIA ATOA AGIZO LA KUACHILIWA HURU WAFUNGWA KWA SABABU YA CORONA

  • Rais wa Nigeria atoa agizo la kuachiliwa huru wafungwa kwa sababu ya virusi vya Corona
Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria amemtaka Jaji Mkuu wa nchi hiyo awaachilie huru wafungwa ambao wamekuwa wakisubiri kusikilizwa kesi zao kwa kwa muda wa miezi sita sasa au zaidi, kama moja ya njia ya kukabiliana na ueneaji wa virusi vya Corona katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Rais wa Nigeria amenukuliwa akisema kuwa, asilimia 42 ya wafungwa 74,000 wamekuwa wakisubiri kusikilizwa kesi zao, hivyo amemtaka Ibrahim Tanko Muhammad Jaji Mkuu wa nchi hiyo awaachilie huru wafungwa hao na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika magereza ya nchi hiyo hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na virusi vya Corona.
Rais Buhari ameeleza katika agizo lake hilo kwamba, msamaha huo utawahusu wafungwa wanaokabiliwa na kesi ambazo sio za jinai, wenye umri mkubwa na wanaogua maradhi mbalimbali.
Agizo hilo linajiri wiki mbili tu baada ya agizo jingine kama hilo ambapo Rais Buhari alitaka kuachiliwa huru wafungwa 2,600 wenye umri wa miaka 60 na zaidi, wanaogua maradhi hatari na wale ambao wamebakiza miezi sita tu kabla ya kumaliza vifungo vyao na ambao kimsingi walihukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu au zaidi.
Walimwengu wameendelea kuitaka serikali ya Nigeria imuachilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky
Hivi karibuni, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) ilitoa wito wa kuachiwa huru kiongozi wake, Sheikh Ibrahim Zakzaky anayekabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya corona akiwa kizuizini, takwa ambalo hata hivyo bado halijatekelezwa na serikali ya Rais Buhari.
Licha ya Mahakama Kuu ya Nigeria kuwahi kutoa hukumu iliyosisitiza kuwa Sheikh Zakzaky pamoja na mkewe hawana hatia yoyote na ikaamuru waachiliwe huru, lakini wawili hao wangali wameendelea kuwekwa jela licha ya hali zao za afya kuwa mbaya sana, tangu walipotiwa nguvuni mwaka 2015 baada ya jeshi la Nigeria kushambulia Husseiniya ya Baqiyatullah katika mji wa Zaria huko Kaduna.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana