Featured

    Featured Posts

VYAMA 200 DUNIANI VIMESAINI TAARIFA KWA KUSHIRIKIANA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Vyama 200 duniani vimesaini taarifa kwa ajili ya kushirikiana dhidi ya virusi vya corona
Harakati ya An Nahdhah ya Tunisia imetangaza kuwa zaidi ya vyama 200 duniani vimesaini taarifa kwa lengo la kushrikiana katiak mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona
Harakati ya An Nahdhah ya Tunisia imeeleza kuwa harakati hiyo pamoja na vyama zaidi ya 200 kote ulimwenguni vikiwemo chama tawama cha Afrika Kusini cha African National Congress(ANC), chama cha Uadilifu na Ustawi cha Uturuki na chama cha Umoja cha Russia vimesiistiza katika taarifa yao ya pamoja juu ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona. Kwa mjibu wa taarifa hiyo ya An Nahdhah, vyama hivyo vimeazimia kwa dhati kukabiliana na virusi vya corona katika wakati huu nyeti kwa kufanya uratibu madhubuti na kuwajibika kwa jadi. 
Wananchi wakidhibti maambukizo ya virusi vya corona 
Vyama hivyo zaidi ya 200 kote duniani aidha vimezitolea wito nchi zote duniani kutoa kipaumbele kwa suala la usalama na afya ya wananchi wao na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na maambukizi ya corona. 
Vyama vikuu katika nchi mbalimbali duniani vimesisitiza kuwa vinaunga mkono kuboreshwa ubadilishanaji wa taarifa kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya corona na kushirkiana katika sekta ya tiba ikiwemo kushauriana kwa pamoja ili kufanikisha utengenezajiwa dawa na chano dhidi ya virusi vya corona; na vile vile kutoa huduma za kiufundi na kifedha kwa nchi zinazohitaji. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana