Featured

    Featured Posts

RWAND YAONGEZA WIKI MBILI KUTOTOKA NJE

Serikali ya Rwanda imeogeza kwa karibu wiki mbili amri ya kutotoka nje hadi Aprili 30 kama sehemu ya hatua ya kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Hii ni hatua ya pili kali kutangazwa na serikali wiki mbili baada ya amri ya kwanza ya kutotoka nje kutangazwa ghafla usiku wa Machi 21 na kuanza kutekelezwa asubuhi yake.

Wakati huo Rwanda ilikuwa imeripoti kuwa na wagonjwa 17 pekee wa orona, lakini idadi hiyo siku ya Ijumaa iliongezeka hadi 138, huku watu 60 wakithibitishwa wakipona.

Virusi vya Corona: Jinsi marufuku ya misongamano inavyokumbana na vikwazo Afrika
Watu wanaruhusiwa kutoka majumbani mwao wakati wanapoenda kutafuta huduma za kimatibabu,chakula, huduma za kifedha au kutoa huduma hizo.

Wafanyabiashara wadogo wameathiriwa zaidi na hatua hiyo; baadhi yao wamesimulia BBC jinsi maisha yalivyokuwa magumu wiki mbili za kwanza.

Mamlaka nchini Rwanda imesema kuwa itaendelea kutoa msaada wa chakula kwa watuwasiojiweza japo idadi ya watu hao imekuwa kubwa zaidi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana