Featured

    Featured Posts

UFARANSA YAAHIDI KUISAIDIA TANZANIA, AFRIKA KATIKA MAPAMBANO YA CORONA


Na Said Mwishehe, Michuzi TV


UFARANSA imesema kuwa  imeadhimia zimia kuisaidia Afrika na Tanzania katika mapambana na maambukizi ya Covid-19 huku ikisisitiza kuwa imeweka nguvu zaidi kwenye ambazo ziko hatarini zaidi.

Kwa mujibu wa Ufaransa ni kwamba Aprili 8 mwaka huu kupitia Rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron ilitangaza kutoa msaada wa Sh.Euro bilioni 1.2 ili Kupambana na maambukizi ya Covid-19 katika Bara la Afrika.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kitengo Cha Mawasiliano cha  Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania imeeleza kwa kina kuhusu nchi hiyo ilivyodhamiria kulisaidia Afrika na Tanzania dhidi ya ugonjwa huo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Claivier kupitia taarifa hiyo amesema nchi ya
Ufaransa imeamua kutumia njia mbalimbali zinazowezekana ili kulisaidia bara la Afrika na haswa nchi zilizo hatarini zaidi ili kupigana vita dhidi ya virusi vya COVID-19 na kuzuia
kutetereka kwa uchumi katika bara la Afrika.  

"Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza Aprili 8, 2020 kutoa msaada wa pesa kiasi cha Euro (€) bilioni 1.2 ili kupambana na maambukizi ya Covid-19
barani Afrika. Huu mpango wa  "COVID-19 - Afya kwa Pamoja",  unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa
(AFD) utakusudia kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na kuwajengea uwezo wanasayansi wa kiafrika katika kufanya gunduzi na tafiti mbalimbali za kisayansi. 

"Hatua hii haitatoa tu majibu ya haraka ya changamoto za kiafya za muda mfupi (short-term), lakini pia itawajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kijamii na jinsi ya kujiandaa baada ya changamoto hizo kuisha. Sambamba na juhudi hizi, Rais wa Ufaransa na serikali yake amekuwa mstari wa mbele kulitetea bara la Afrika ili lipewe kipaumbele katika kupata misaada kutoka umoja wa nchi za Ulaya na taasisi mbalimbali za kimataifa,"amesema Balozi Claivier. 

Ameongeza kuwa Ufaransa inashika namba tano ulimwenguni kwa kutoa misaada kwa wingi, ikiwa imetoa misaada ya maendeleo kwa jamii ambayo ilikuwa karibu kiasi cha Euro (€) bilioni 11 mwaka wa 2019 na kuongeza katika kupambana na janga la Covid-19, Ufaransa itatoa misaada mbalimbali ikishirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa ili kuiunga mkono Afrika katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona.
 
"Uhamasishaji wa muda mrefu wa Ufaransa katika kuisaidia Afrika katika nyanja mbalimbali bado utaendelea kama kawaida. Kati ya programu zingine, Ufaransa ni
mchangiaji wa 5 katika kuchangia kiasi kikubwa katika chama cha Kimataifa cha Maendeleo (International Development Association) ambacho kimekusanya dola za kimarekani bilioni 14 ili kukabiliana na dharura ya mlipuko wa Covid-19 

"Na pia kimechangia kiasi cha dola za kimarekani bilioni 160 katika mpango wa muda wa kati (medium-term plan) katika kusaidia uchumi; pia Ufaransa ni mchangiaji wa pili wa kihistoria katika mfuko wa "global fund" mfuko ambao umeandaa utaratibu maalum kwaajili ya kupambana na janga la  Covid-19,"amesema.

Balozi huyo ameongeza katika mfuko huo Ufaransa ilitoa dola za kimarekani milioni 500 na kwamba Ufaransa ni mchangiaji wa sita(kwa wingi wa fedha inazotoa) kwa  Shirika la Afya Duniani(WHO) ikichangia upande wa bajeti ya lazima (karibu Euro milioni 20 kwa mwaka).

Pia  ni mchangiaji wa kwanza (kwa kiwango cha fedha) kwa shirika liitwalo Unitaid. Ufaransa pia ni mchangiaji namba 2 (kwa wingi wa fedha itolewayo kama mchango) kwa umoja wa Ulaya, ambayo ilitangaza msaada wa kifedha kwa nchi washirika kiasi cha euro (€) bilioni 15.6.
Katika hatua nyingine.

" Rais Macron alibeba jukumu la kuratibu mpango wa kusitishwa kwa deni kwa nchi za Kiafrika. Mnamo Aprili 14, mwakanhuu, Ufaransa ilipata kutoka kwa washirika wake,
kupitia mfumo wa klabu ya Paris (Paris Club) na nchi za G20, kusitisha kwa riba ya madeni katika nchi zinazoendelea (jumla ya nchi zilizopata nafuu hiyo ni nchi 70, kati ya hizo 40 zinapatikana kusini mwa jangwa la Sahara).

" Kati ya jumla ya dola za kimarekani bilioni 32 katika msamaha wa madeni, Ufaransa pamoja na washirika wake walifanikisha kusitishwa kwa deni ambalo ni jumla ya dola za kimarekani bilioni 20 na wataendelea na utetezi huu, ikiwa ni pamoja na kupendekeza urekebishaji au hata kufutwa kwa deni, "amesisitiza Balozi Claivier kwenye taarifa hiyo.

Pamoja na hayo, amesema Ubalozi wa Ufaransa tayari unaunga mkono kwa dhati kabisa katika juhudi za kitaifa za mapambano dhidi ya
Covid-19 pamoja na madhara yatokanayo na virusi hivyo .

Wakati huo huo amesema mradi wake unaoendelea wa kilimo-ekolojia, unaotekelezwa na taasisi ya SwissAid pamojana asasi zisizo za kiserikali (NGOs) za Kitanzania ambazo ni SAT na TOAM zinalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wapatao 6000, lengo likiwa kuzuia magonjwa ya mlipuko kwa watu waishio vijijini.

" Kiasi Cha Euro 500,000 zitaelekezwa katika jitihada za kupambana na magonjwa ya mlipuko, kuhakikisha uwepo wa akiba ya chakula na kutoa msaada wa kiuchumi kwa jamii za watu waishio vijijini na walio katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

"Pamoja na shughuli zake za kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya na maji
nchini Tanzania (karibu Euro milioni 310 iliyojitolea zaidi ya miaka 10 iliyopita), AFD tayari inafanya kazi bega kwa bega na serikali na NGOs mbalimbali ili kutathmini uwezekano wa kupata tena fedha za ruzuku (karibu Euro (€) 500,000) ili kuweza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya pamoja na kusambaza vifaa tiba," amesema.

Pia kama sehemu ya Mpango wa "COVID-19 - Afya kwa Pamoja", AFD imeahidi kuunga mkono serikali ya Tanzania kupitia mikopo yenye masharti nafuu ili kuiwezesha serikali kushughulikia changamoto za kiafya za muda mafupi na mda wa kati.

Balozi huyo wa Ufaransa nchini Tanzania pia alihamasisha kampuni za Ufaransa zilizopo nchini Tanzania kuunga mkono na kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vya corona kwa kutoa vifaa vinavyohitajika ili kupambana na ueneaji wa janga hili la corona.
 
 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Claivier  
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana