Alisema ni wajibu wa kila mmoja kuunganisha nguvu katika kuhakikisha kuwa jamii inasaidiwa kuondokana na janga hili bila kujali itikadi za vyama hatua ambayo itawezesha Tanzania kubaki salama.
“Tumekabidhi vifaa hivi msahususi ambavyo vitagawiwa katika wilaya zote tano za Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhakikisha tunaendelea kujikinga na kuzingatia ushauri wa wataalamu wetu, ambapo vitaenda kwenye katika jamii yetu ikiwamo, watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, bodaboda, yatima, masoko na makundi mengine kwani tunaamini kila mtu ana haki ya kuthaminiwa.
“Hivyo, tumeona tuiunge mkono Serikali na tuungane na Rais wetu Dk. John Magufuli kwenye vita hii ya corona, tunaamini kuwa tunapitia katika kipindi kigumu lakini silaha kubwa ni kuwa wamoja katika kipindi hiki kwa kuacha itikadi zetu za vyama na mambo mengine na tukaungana kama taifa wakubwa na wadogo katikia vita hii naamini tutavuka salama.
“Hivyo vifaa hivi ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh milioni nne tutavigawa kwenye wilaya hizo kupitia Umoja wa Vijana,” alisema Kilakala.
Upande wake Katibu wa Hamasa wa umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Ally Ummy, alisema kuwa wameona ni vyema kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukata mnyororo wa maambukizi ya corona katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Vifaa hivi vinaenda sambamba na kauli mbiu yetu ya ‘Uimara wa afya yako, Uimara wa Taifa lako, Tutaishinda corona, Tutavuka salama’, hivyo lengo la vifaa hivi ni kwenda kuelimisha wananchi kwenye Wilaya ya Kata zenu juu ya matumizi sahihi ya vifaa hivi ili kusaidia kuepusha maambukizi,” alisema Mhandisi Ummy.
Post a Comment