Featured

    Featured Posts

ZIJUE NCHI 15 DUNIANI ZISIZOKUWA NA WAGONJWA WA CORONA

Tarehe 12 Januari chini ya miezi minne iliyopita - virusi vya corona vilikua ndani ya Uchina pekee. Hapakuwa na mgonjwa hata mmoja aliyekuwa amepatikana nje ya nchi hiyo ambayo virusi hivyo vilianzia.
Siku moja mbele yaani Januari 13, virusi hivyo vikaanza kuwa tatizo la dunia. Mgonjwa wa kwanza alirekodiwa Thailand kisha Japani, Korea Kusini zikafuatia haraka.
Katika maeneo mbalimbali ya dunia wakaanza kuongezeka.
Kufikia sasa zaidi ya watu zaidi ya milioni 2.9 wamethibitishwa kuugua corona duniani kote kutoka nchi kama Nepal mpaka Nicaragua.
Lakini je wakati idadi ya vifo ikiongezeka, na hospitali zikifurika wagonjwa, bado kuna nchi ambazo hazina kabisa wagonjwa wa virusi vya corona?
Jibu huenda likakushangaza, NDIO!
Kuna nchi 193 ambazo ni wanachma wa Umoja wa Mataifa.
Kufikia Aprili 26 nchini 15 zilikua hazijaripoti mgonjwa hata mmoja wa virusi vya corona, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Nchi 15 zisizo na Covid-19
Visiwa vya Comoro; Kiribati; Lesotho; Visiwa vya Marshall; Micronesia; Nauru; Korea Kaskazini; Palau; Samoa; Visiwa vya Solomon; Tajikistan; Tonga; Turkmenistan; Tuvalu na Vanuatu.
Hivyo barani Afrika kuna nchi mbili tu ambazo mpaka sasa hazina mgonjwa wa corona hata mmoja nazo ni Visiwa vya coromo na Lesotho.
Baadhi ya wataalamu wanaafiki kuwa nchi hizi zinaweza kuwa na wagonjwa ambao hawajaripotiwa.
Korea Kaskazini kwa mfano, hakuna hata mgonjwa mmoja aliyeripotiwa jambo wataalamu wanamashaka na hilo.
Lakini kuna nchi ambazo virusi havijafika.
Vingi kati ya visiwa vidogo vyenye wageni wachache - saba kati ya visiwa 10 ambavyo havitembelewi duniani kulingana na data za Umoja wa Mataifa, viko huru na Covid-19.
Umbali wake na maeneo mengine - unamaanisha kuwa kanuni ya kutochangamana tayari ndiyo maisha wanayoishi.
Hata hivyo rais wa moja ya visiwa hivyo ameimambia BBC kuwa Covid-19 ni jambo la dharura kwao.
Nauru, kisiwa kilichopo katika bahari ya Pasfiki, kiko takriban maili 200 (320 km) kutoka eneo lolote jingine - Kisiwa cha Banaba, sehemu ya Kiribati, ni kisiwa kilichopo karibu zaidi. Mji mkubwa uliopo karibu ni Brisbane, ambao upo maili 2,500 kusini magharibi.
Kisiwa hiki kina takriban watu 10,000, ikiwa ni idadi ndogo zaidi baada ya ile ya wakazi wa Tuvalu.
Ni moja ya maeneo ambayo yanatembelewa na watu wachache zaidi duniani ingawa hakionekani kwenye data za hivi karibu za Umoja wa Mataifa. Mmoja wa wanaoendesha biashara ya utalii nchini humo anasema kisiwa hicho kwa mwaka kinapokea watalii 160 tu.
Unaweza kudhani kuwa maeneo hayo ya mbali kiasi hicho hayahitaji kujitenga zaidi. Lakini nchi yenye hospitali moja, bila mashine za kusaidia wagonjwa kupumua na ukosefu wa wauguzi haziwezi kuacha kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi.
  • Katikati ya mwezi Machi, Nauru Airlines ilisitisha safari za ndege za kuelekea Fiji, Kiribati na Visiwa vya Marshall na kupunguza safari za kuelekea - Brisbane - kutoka mara tatu mpaka mara moja kwa wiki.
  • Baadha ya hapo wale waliokua wanawasili kutoaka Australia waliamrishwa kujitenga katika karantini kwa wiki 1 katika hoteli.
Sera hiyo, anasema rais Lionel Aingimea, inaitwa "Kuzuiwa kwa Maambukizi".
"Tunazuia maambukizi mipakani, anasema rais.
"Tunatumia uwanja wetu wa ndege kama mpaka."
Wale waliowekwa karantini huchunguzwa iwapo wanadalili kila siku. Pale ambapo baadhi hukutwa na homa hutengwa zaidi na kupimwa ugonjwa wa Covid-19. Mpaka kufikia sasa vipimo vyote vilivyopelekwa Australia, vinaonesha kwamba hakuna mtu mwenye maambukizi.
Licha ya kuishi katika kipindi hiki cha janga, wananchi wa kawaida wa Nauru "wako katika hali tulivu", anasema rais.
"Tulipoanzisha sera hii ya karantini nilimuomba Mungu na akanipa aya ambayo nimeitunza moyoni mwangu nayo ni Zaburi 147, mstari wa 13 na 14. Hiyo imenitia nguvu wakati tunapopitia hali - kama Biblia inavyosema -hili bonde la mauti."
Na huku akijaribu kuizuwia Nauru kupata maambukizi ya Covid-19, anafahamu fika kuwa maeneo mengine ya dunia hayana bahati kama hiyo.
"Kila mara tunapoiangalia ramani ya [Covid-19] inaonekana kana kwamba dunia imekumbwa na mlipuko wa surua - kuna alama nyekundu kila mahali,"anasema
"Kwa hiyo tunaamini kuwa maombi yetu kama taifa …tunaamini yatasaidia mataifa mengine yanayopitia vipindi hivi vigumu."
Nauru sio kisiwa pekee kidogo kilichoko katika bahari ya Pasifiki kilichotangaza hali ya dharura - Kiribati, Tonga, Vanuatu, na visiwa vingine wamefanya hivyo.
Dkt Colin Tukuitonga, kutoka Niue Pasiifik Kusini, ana uhakika kuwa ni sera sahihi.
" Kazi yao kubwa bila shaka ni kuhakikisha jinamizi hilo haliingii kwao ," amesema hayo kutoka New Zealand. "Kwasababu likiingia watakua wamepatikana, kusema kweli ."
Dkt Tukuitonga ni mtaalamu wa afya ya umma , kamishna wa zamani wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa na sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Auckland
Na amesema pia kwamba wakazi wengi wa visiwa vya Pacific tayari wana afya duni.
"Maeneo haya mengi yana viwango vikubwa vya visa vya ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo na kifua-yote haya yanahusishwa na dalili mbaya za virusi vya corona ."
Wanahitaji kusalia bila kuwa na kisa hata kimoja cha coronavirus.
'' Kutengwa kwa visiwa vyao vyenye idadi ndogo ya watu vilivyotengwa sana katika bahari kubwa limekua ni tatizo kwao- lakini kwa sasa tatizo hilo limewakinga," he alisema.
Idadi ndogo ya nchi zenye mipaka ya ardhi hadisasa pia havijapatwa na visa vya maambukizi ya coronavirus
Ilikua ni Alhamisi tu ambapo Malawi, nchi isiyopakana na bahari yenye watu milioni 18 Mashariki mwa Afrika , iliporipoti kisa chake cha kwanza. Lakini ilikua imejiandaa kwa virusi hivyo.
Nchi hiyo ilikua imetangaza "maafa ya kitaifa", ilifunga shulle na kufuta vibali vyote vya safari( Viza) kabla ya tarehe 20 Machi. Pia ilianza kupima anasema Dkt Peter MacPherson, katika taasisi ya mataalamu wa afya ya umma katika taasisi ya Liverpool School ya dawa za magonjwa ya maeneo ya jito, ambaye kazi yake inadhaminiwa na wakfu wa Wellcome anayeishi nchini Malawi.
Anasema wiki moja au mbili zaidi t''umekuwa tukijiandaa'' na anaamini kuwa Malawi itakabiliana na virusi.
"Tumekua tukiathiriwa sana na janga la HIV kwa miaka 30 iliyopita na pia kifua kikuu," anasema.
Ushahidi unaonyesha kuwa coronavirus itakwenda katika kila nchi, anasema Dkt MacPherson. Kwa hiyo sio Malawi, ni eneo gani ambalo litakua la mwisho duniani kupata Covid-19 ?
"Kuna uwezekano mkubwa kuwa zitakua ni nchi hizo za Pacific Kusini , visiwa vilivyo maeno ya mbali ,ninaweza kubeti kwa pesa kuhusu hilo ," anasema Andy Tatem, Profesa wa masuala ya idadi ya watu na maeneo yao na magonjwa ya majanga katika Chuo Kikuu cha Southampton.
"Lakini katika uchumi wetu wa utandawazi, sina uhakika iwapo kuna kokote kutakakoepuka ugonjwa wenye maambukizi wa aina hiyo ."
Sheria za kutotoka nje kama -ile iliyowekwa Nauru - zinaweza kuwa na ufanisi, anasema, lakini haziwezi kudumu daima.
"Nyingi kati ya nchi hizi zinategemea kiasi Fulani cha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje -ziwe za chakula au bidhaa nyingine pamoja au utalii. Inawezekana kuwa wanaweza kujifungia kabisa, lakini itawaletea athari mbaya-na hatiamae watalazimika kufungua mipaka yake ."
Na ameonya kuwa, idadi ya visa haijapanda bado.
"Sote tuna hizi sheria za kukaa nyumbani , kwa hiyo bado virusi havijasambaa kwa miongoni mwa watu sanana bado tuna watu wengi ambao hawajapata maambukizi.
"Ni vizuri kwa mifumo ya afya, lakini hii ina maanisha kuwa bado tuna watu wengi duniani wanaoweza kupatwa na maambukizi . Tutaishi na virusi hivi kwa muda ."

Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 22 Aprili 2020

Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
Jumla ya visa vilivyothibitishwa Jumla ya vifo
2,524,433 177,503
Visa Vifo
Marekani 824,065 44,996
Uhispania 204,178 21,282
Italia 183,957 24,648
Ujerumani 148,453 5,086
Uingereza 129,044 17,337
France 117,324 20,796
Uturuki 95,591 2,259
Iran 84,802 5,297
Uchina 83,864 4,636
Urusi 52,763 456
Brazil 43,368 2,761
Belgium 40,956 5,998
Canada 39,405 1,915
Netherlands 34,139 3,916
Uswizi 28,063 1,478
Ureno 21,379 762
India 20,111 645
Peru 17,837 484
Ireland 16,040 730
Sweden 15,322 1,765
Austria 14,873 491
Israel 13,942 184
Saudi Arabia 11,631 109
Japan 11,512 281
Chile 10,832 147
Korea Kusini 10,694 238
Ecuador 10,398 520
Poland 9,856 401
Kashmir inayotawaliwa na Pakistan 9,749 209
Mexico 9,501 857
Romania 9,242 498
Singapore 9,125 11
Milki za Kiarabu 7,755 46
Denmark 7,695 370
Norway 7,241 182
Indonesia 7,135 616
Jamuhuri ya Czech 7,033 201
Belarus 6,723 55
Australia 6,647 74
Serbia 6,630 125
Ufilipino 6,599 437
Qatar 6,533 9
Ukrain 6,125 161
Malaysia 5,482 92
Jamuhuri ya Dominica 5,044 245
Panama 4,821 141
Colombia 4,149 196
Finland 4,014 141
Luxembourg 3,618 78
Misri 3,490 264
Afrika Kusini 3,465 58
Bangaldesha 3,382 110
Morocco 3,209 145
Argentina 3,144 151
Thailand 2,826 49
Algeria 2,811 392
Moldova 2,614 72
Ugiriki 2,401 121
Hungary 2,168 225
Kuwait 2,080 11
Kazakhstan 2,025 19
Bahrain 1,973 7
Croatia 1,908 48
Iceland 1,778 10
Uzbekistan 1,692 6
Iraq 1,602 83
Estonia 1,552 43
Oman 1,508 8
Azerbaijan 1,480 20
New Zealand 1,451 14
Armenia 1,401 24
Lithuania 1,370 38
Slovenia 1,344 77
Bosnia na Herzegovina 1,342 51
Macedonia Kaskazini 1,231 55
Slovakia 1,199 14
Cameroon 1,163 43
Cuba 1,137 38
Afghanistan 1,092 36
Ghana 1,042 9
Bulgeria 1,015 47
Djibouti 945 2
Cote d'voire 916 13
Puerto Rico 915 64
Tunisia 901 38
Cyprus 784 12
Nigeria 782 25
Latvia 748 9
Andorra 717 37
Mili ya Diamond Princess 712 13
Guinea 688 6
Lebanon 677 21
Costa Rica 669 6
Niger 657 20
Kyrgystan 612 7
lbania 609 26
Bolivia 609 37
Burkina Faso 600 38
Uruguay 543 12
Kosovo 510 12
Honduras 510 46
San Marino 476 40
Maeneo ya Wapalestina 466 4
Malta 443 3
Jordan 428 7
Taipei ya China 425 6
Senegal 412 5
Kisiwa cha Reunion 410
Georgia 408 4
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo 350 25
Mauritius 328 9
Guatemala 316 8
Montenegro 313 5
Mayotte 311 4
Sri Lanka 310 7
Isle of Man 307 9
Kenya 296 14
Venezuela 288 10
Somalia 286 8
Vietnam 268
Mali 258 14
Jersey 255 14
Tanzania 254 10
Guernsey 241 10
Jamaica 233 6
El Salvador 225 7
Paraguay 213 9
Visiwa vya Faroe 185
Congo 165 6
Martinique 164 14
Gabon 156 1
Rwanda 150
Guadeloupe 148 12
Sudan 140 13
Brunei Darussalam 138 1
Guam 136 5
Gibraltar 132
Cambodia 122
Myanmar 121 5
Madagascar 121
Trinidad and Tobago 115 8
Ethiopia 114 3
Liberia 101 8
Bermuda 98 5
Guiana ya Ufaransa 97 1
Aruba 97 2
Monaco 94 3
Maldivers 86
Togo 86 6
Equitorial Guinea 83
Liechtenstein 81 1
Barbados 75 5
Zambia 70 3
Cape Verde 68 1
Netherlands Antilles 68 10
Visiwa vya Cayman 66 1
Guyana 66 7
Bahamas 65 9
Uganda 61
Libya 59 1
Haiti 58 4
Polynesia ya Ufaransa 57
Benin 54 1
Visiwa vya Virgin vya Marekani 53 3
Sierra Leone 50
Guinea_Bissau 50
Nepal 42
Syria 42 3
Mozambique 39
Eritrea 39
Saint Martin (Eneo la Ufaransa) 38 2
Mongolia 35
Chad 33
Eswatini 31 1
Zimbabwe 28 3
Antigua na Barbuda 24 3
Angola 24 2
Timor_Leste 23
Botswana 20 1
Jamuhuri ya kidemokraia ya watu wa Lao 19
Malawi 18 2
New Caledonia 18
Belize 18 2
Fiji 18
Namibia 16
Dominica 16
Saint Lucia 15
Saint Kitts na Vevis 15
Netherlands Antilles 14 1
Visiwa vya Kaskazini vya Mariana 14 2
Jamuhuri ya Afrika ya Kati 14
Grenada 14
St St Vincent na Gradines 13
Montserrat 11
Visiwa vya Falkland 11
Turks nad Visiwa vya Caicos 11 1
Greenland 11
Burundi 11 1
Ushelisheli 11
Suriname 10 1

Gambia 10 1
Nicaragua 10 2
Vatican 9
Mili ya MS Zaandam 9 2
Papua News Guinea 7
Mauritania 7 1
Bhutan 6
Saint Barthélemy 6
Milki ya Magharibi mwa Sahara 6
Visiwa vya Virgin vya Uingereza 5 1
Sudan Kusini 4
Sao Tome and Principe 4
Anguilla 3
Yemen 1
Saint Pierre na Miquelon 1

Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins, maafisa wa eneo
Mara ya mwisho kufanyiwa mabadiliko 22 Aprili 2020, 07:00 GMT +1.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana