Featured

    Featured Posts

BARAZA LA USALAMA LA UN LAJARIBU KUKUBALIANA KUHUSU AZIMIO LA COVID-19

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajaribu tena kufikia makubaliano katika azimio lake la kwanza tangu janga la virusi vya corona kuanza duniani zaidi ya miezi miwili iliyopita, lakini mzozo kati ya Marekani na China kuhusiana na kulitaja shirika la afya ulimwenguni WHO bado haujatatuliwa.

Marekani siku ya Ijumaa ilipinga pendekezo la azimio lililotayarishwa na Ufaransa na Tunisia baada ya wanadiplomasia kusema wamekubaliana na lugha iliyotumika na China ambayo haitaji moja kwa moja shirika hilo la afya la Umoja wa mataifa.


Balozi wa Urusi Vassily Nebenzia amesema kuna makubaliano katika karibu kila sehemu ya azimio hilo, lengo kuu likiwa ni kuunga mkono wito wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres wa Machi 23 kwa dunia kuwa pamoja ili kupambana na janga la COVID-19.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana