Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne,watatu wakiwa familia moja kwa tuhuma za kumuuwa kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni na sehemu za siri Baba yao Lumba Nhalima(57).
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wakati marehemu akitoka kunywa pombe na kuelekea nyumbani.
Akithibitisha tukio hilo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga alisema, siku ya tukio watuhumiwa walimnywesha pombe nyingi marehemu ili ashindwe kujitambua kwa lengo la kumdhuru.
Kwa mujibu wa kamanda Kuzaga ni kwamba,marehemu akiwa njiani kurudi nyumbani alikutana na watuhumiwa hao ambao ni Sali Lumba(32) Jonas Lumba(28) na Paulo Lumba(19) na mtu mwingine ambaye alikuwa anakunywa naye pombe marehemu aliyetambulika kwa Thomas Malongo(54)
Kuzaga alisema, baada ya uchunguzi jeshi la Polisi limebaini kuwa, kabla ya kifo chake marehemu alikuwa akilalamika kuwa watoto wake wan ne ambao ni wa mke mkubwa aitwaye Wande Mabuki(46)wanataka kumuuwa ili yeye na watoto warithi mali zake.
Hata hivyo Kuzaga alisema, chanzo cha kifo hicho kinahusishwa nan a Imani za kishirikina pampja na tamaa za kurithi mali, kwa hiyo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio hilo.
Aidha Kamanda Kuzaga amesema, baada ya mahojiano ya kina watuhumiwa hao wanne wamekiri kuhusika kupanda njama na kufanikisha mauaji.
“jeshi la polisi linatoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kuachana na dhana potofu za kujipatia kipato kwa njia ambazo si halali ikiwemo njia za kishirikina” alisema Kamanda Kuzaga.
Post a Comment