Featured

    Featured Posts

DC LUDEWA AWASISITIZA WAZAZI KUHAKIKISHA WATOTO WAO WANAPATA ELIMU BORA


 Mkurugenzi wa taasisi ya PADECO akikagua vyumba vya jengo la utawala.
 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere (kulia) akikagua jengo la utawala linaloendelea kujengwa

 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Adrea Tsere(Kushoto) akielekezwa ramani ya ujenzi wa shule ya Nicopolis Academy, kulia ni mmiliki wa shule hiyo Augustino Mwinuka
 Diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchiro(kulia) akiangalia vyumba vya madarasa ambavyo vinaendelea kujengwa
 
Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsere amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu bora ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na kufikia kiwango cha kati. 

Hayo aliyasema alipotembelea mradi wa ujenzi wa shule ya Nicopolis Academy inayomilikiwa na Augustino Mwinuka nakujengwa chini ya ufadhilii wa prof Ludwig Gernhardt kutoka ujerumani kupitia taasisi ya Participatory Development Concern (PADECO). 

Alisema kuwa vizazi vya sasa vinahitaji elimu zaidi ili kuweza kubadilisha maisha kutoka katika hali duni na kuwa na maisha bora. 

“Ili tuendane na sera ya viwanda tunapaswa kuwajenga watoto wetu katika elimu zaidi kwakuwa bila elimu hatuwezi kuwa na maarifa ya kuanzisha viwanda”. Alisema Tsere. 

Naye Diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchiro amempongeza mmiliki wa shule na kusema kuwa itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa shule huku akiahidi kumuunga mkono katika kuboresha miundombinu ya barabara . 

Alisema ataongea na wananchi ili waungane kwa pamoja katika kuboresha miundombinu ya barabara hiyo inayoelekea shuleni hapo na kuwarahisishia watoto watakaosoma hapo kupita kwa urahisi. 

Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa Padeco Willbad Mwinuka Amesema kuwa ujenzi huo ni mwanzo wa maendeleo zaidi kwakuwa baada ya kukamilisha majengo hayo ni matarajio yao kuendelea kufanya ujenzi wa shule nyingine katika maeneo mbalimbali. 

Aliongeza kuwa shule hiyo itawasaidia watoto wasiyo jiweza na waishio katika mazingira magumu lakini pia kwa wale wenye uwezo watakaohitaji watoto wao wasome hapo watalazimika kuchangia gharama kidogo. 

Ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi Desemba Mwaka huu na majengo hayo kuanza kutumika mwezi January mwaka ujao ikiwa na vyumba nane vya madarasa, jengo la utawala, jengo la waalimu, mabweni ya wanafunzi pamoja na matundu ya vyoo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana