Makamu wa Rais Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA). Ibrahim Mgoo akizungumza jambo leo Mei 12, 2020 ikiwa ni kumbukizi ya Madhimisha ya miaka 200 tangu kuzaliwa kwa mwasisi wa Uuguzi Duniani Bi.Florence Nightingale. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Niwaase Wasanii na watu wengine maarufu kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya badala ya kuwatisha kuwa Wauguzi ni watu wabaya Kama alivyofanya msanii mmoja hivi alipomwambia mke wake wakati anaenda kujifungua kuwa aende akapambane na Wauguzi, hii siyo sahihi.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Ibrahim Mgoo wakati alipokuwa akizungumza nami kuekeke kumbukizi ya kuzaliwa Mwasisi wa taaluma hii Bi.Florence Nightingale nakusherehekea siku ya Uuguzi mahala pa kazi kutokana na ugojwa wa homa Kali ya Mapafu (Covid-19). alisema Mgoo.
Ni siku ya Wauguzi Duniani lakini pia mwaka 2020 umetangazwa kuwa ni mwaka wa Muuguzi na mwaka huu tunaadhimisha miaka 200 tangu kuzaliwa kwa mwasisi wa Uuguzi Duniani Bi.Florence Nightingale.
Ni mwaka ambao ulipeba Mambo mengi kuhusu Uuguzi, lengo likiwa ni kuinua hadhi ya Uuguzi Nchini na Duniani kote.
Kutokana na Changamoto ya kuenea kwa homa Kali ya Mapafu (Covid-19) hatutakuwa na maadhimisho hayo kwa kusherehekea Kama ilivyoada bali tutaendelea na utoaji wa huduma za kiuguzi katika maeneo yote ya kutolea huduma za kiuguzi Nchini huku tukikumbuka matendo mema ya mwasisi wa taaluma hii Bi. Florence Nightingale.
Jamii inapaswa kutambua mchango wa Muuguzi na kuondoa Imani potofu kuwa Wauguzi ni watu wabaya.
Pia niendelee kuwaasa Wasanii na watu wengine maarufu kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya badala ya kuwatisha kuwa Wauguzi ni watu wabaya Kama alivyofanya msanii mmoja hivi alipomwambia mke wake wakati anaenda kujifungua kuwa aende akapambane na Wauguzi, hii siyo sahihi.
Nitumie fursa hii kumpongeza Rais wetu mpendwa Mh.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea kuwatambua Wauguzi, maana katika kila hotuba zake akizungumzia mapambano ya Covid-19 amekuwa akiwapongeza.
Viongozi wengine wanapaswa kuiga hili.
Na tunaendelea kushirikiana na Serikali katika Vita ya Covid-19 kwa kuwahudumia walioathirika kwa homa hii na kuwakinga wengine wasipatwe na Ugonjwa huu ikiwemo sisi wenyewe Kama Wauguzi na familia zetu kwa kuendeleza Elimu ya Afya kwa jamii.
Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sofia Sanga akizungumza nami alisema;.
Nianze kwa kumshukuru Mungu kutupigania katika Afya njema kufikia siku ya leo pia nipende kumpongeza Rais John Pombe Joseph Magufuli kwakutujali na kuthamini mchngo wetu
Sisi wauguzi tuko kwa ajili ya jamii, wateja wetu watuelewe, tunahitaji watuelewe.. jukumu Letu ni kuwajali na kuwahudumia kwa upendo...
Changamoto ya lugha chafu na za kuudhi sio ya kiuuguzi ni tabia ya mtu
sisi tunafundishwa maadili ya kazi yetu ambayo yanatukata kuwahudumia wagonjwa kwa kuzingatia maadili hayo: usawa, ukweli, haki na usawa, kutunza siri za mgonjwa na kumuheshimu.
Wito wangu: ni kuwa wauguzi tunapotoa huduma tuzingatie utu na thamani ya kila mtu anayefika mbele yetu.
Wauguzi: mbiu inayoongoza uuguzi kwa dunia yenye afya
Post a Comment