Polisi nchini Marekani wameendeleza vitendo vya kuwabagua Wamarekani wenye asilia ya Afrika na mara hii mwanahabari wa Televisheni ya CNN amekamatwa akiwa anarusha ripoti hewani mubashara kuhusu ghasia za kupinga ubaguzi wa rangi huko Minneapolis.
Kwa mujibu wa taarifa Omar Jimenez, mwanahabari wa CNN alikuwa anarusha hewani ripoti mubashara kuhusu ukatili wa Polisi ya Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wakati alipotiwa mbaroni na polisi.
Katika tukio hilo la Ijumaa Omar Jimenez, ripoti Mmarekani Mwenye Asili ya Afrika akiwa na timu yake walikamatwa na kuzuiwa kurusha hewani ripoti kuhusu ukatili wa polisi ambao umeibua ghasia na machafuko mjini Minneapolis.
Watu wa Minneapolis wanaandamana kupinga ukatili wa polisi wazungu wambao walimuua kinyama Mmarekani mweusi au mwenye asili ya Afrika.
Katika mauaji mapya ya kibaguzi ya polisi wa Marekani Jumatatu iliyopita afisa mmoja wa polisi mzungu alimuua kwa namna ya kikatili George Floyd (46) Mmarekani mwenye asili ya Afrika kwa kumbana shingo kwa goti la mguu wake wa kushoto. Floyd alikuwa akipiga kelele kwa kusema: "Umenibana shingo siwezi kupumua," "naomba maji" na "usiniue" hadi alipofariki dunia. Kufuatia ukatili huo wa kutisha, meya wa mji wa Minneapolis, Jacob Frey amewafuta kazi maafisa wanne wa polisi kwa kusababisha kifo cha Floyd. Kufuatia jinai hiyo, wakazi wa mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota wamefanya maandamano makubwa ya kulaani jinai hiyo huku wakitaka wahusika wachukuliwe hatua kali. Katika maandamano hayo Mmarekani mwingine mweusi ameuawa kwa kupigwa risasi mjini hapo.
Post a Comment