Featured

    Featured Posts

NAIBU SPIKA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA WAUGUZI JIJINI DODOMA




Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Wauguzi katika   Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Baadhi ya Wauguzi wa   Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson   wakati wa kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Wauguzi Duniani.
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akikagua ukarabati uliofanyika katika Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Wakwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akikata utepe kuzindua Wodi ya Upasuaji ya Wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo ilikuwa katika marekebisho wakati wa kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Baadhi ya Wauguzi wa   Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakila kiapo cha utendaji kazi  wakati wa kilele cha  maadhimisho ya wiki ya Wauguzi Duniani.
PICHA NA BUNGE
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana