Yassir Simba, Michuzi Tv
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imewataka maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFG kuzirejesha fedha walizochukua kabla hatia nyingine hazijafuata.
Hatua hiyo imekuja baada ya TAKUKURU kudai Shirikisho limekuwa na matumizi mabaya ya fedha ikiwemo fedha zilizotolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON ya Vijana chini ya Miaka 17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Brig. John Mbungo amesema taasisi hiyo imeamuru maofisa hao wa TFF kurudisha fedha hizo kabla hatua nyingine hazijafata baada ya kupata ushahidi wa nyaraka mbalimbali.
Mbungo amesema, wanajiandaa kuwahoji baadhi ya maofisa wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kwa matumizi mabaya ya fedha ikiwemo fedha zilizotolewa na Raisi Magufuli billioni moja kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana Afrika,U17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.
Amesema,kuna baadhi ya maofisa wengine wa TFF wamehojiwa na baadhi ya nyaraka zimechukuliwa na wale waliobainika kuchukua fedha hizo wana hiari ya kuzirejesha kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.
Sakata la matumizi mabaya ya fedha ndani ya Shirikisho hilo limeibuliwa na moja ya makocha wa Timu za Vijana alipokuwa katika kipindi cha michezo cha TAMASHA LA MICHEZO kinachorushwa na Luninga ya ITV Jumapili iliyopita akiwatuhumu baadhi ya viongozi wa TFF kujinufaisha na fedha hizo na kuwataka TAKUKURU kufanyia uchunguzi suala hilo.
Aidha, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidau jana alizungumza na vyombo vya habari na kuelezea tuhuma hizo ikiwemo matumizi ya Shirikisho hilo kwa fedha wanazozipata kutoka kwa wadau wa mpira pamoja na Shirikisho la Mpira wa Migui Duniani FIFA.
Shirikisho hilo limeingia katika sakata hilo la matumizi mabaya ya fedha ambapo kumekuwa na wingu zito la viongozi wa soka kuingia kwenye kashfa hiyo katika kipindi cha miaka mitano.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo
Post a Comment