Featured

    Featured Posts

NAIBU WAZIRI MGUMBA AKAGUA VITUO VYA AFYA JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akimsikiliza Diwani wa Kata ya Mikese Mhe Mwega .J. Mohamed,wakati wa ziara yake ya kukagua Kituo cha Afya cha Mikese.

Mjumbe wa kamati ya usimamizi wa Kituo cha Afya cha Mikese akimueleza jambo Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Mgumba,(wakwanza) kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro Mhe Kibena Kingo,(wakati )ni diwani wa kata ya Mikese Mhe Mwega .J. Mohamed.

Mbunge wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akikagua kito cha afya cha Mikese kulia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro Mhe Kibena Kingo.
Sehemu ya majengo ya kituo cha afya cha Mikese
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Mgumba akijadiliana jambo na Diwani wa kata ya Mikese Mhe Mwega .J. Mohamed.

******************************

NA FARIDA SAIDY MOROGORO

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi aliyepewa dhamana ya kujenga kituo cha afya cha
mikese kinachogharimu milioni mia nne za kitanzania.

Katika ziara hiyo Mhe Mgumba aliyeambatana na mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro na kamati ya fedha ya wilaya hiyo, lengo likuwa ni kutembelea miradi ya vituo vya afya katika jimbo lake kujionea na kujiridhisha na kazi zinafanywa na wakandarasi waliopewa
dhamana na serikali ya Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha akiwa katika kituo cha afya cha Mikese Mhe Mgumba amesema licha ya mkandarasi kulipwa fedha zote na serikali lakini ameshindwa kumaliza kazi katika kipindi cha mkataba, ambapo mkataba ulimtaka kumaliza kazi mwezi disemba mwaka jana.

Amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya mungano wa watanzania Dkt John Pombe Magufuli imesogeza huduma za kijamii karibu na wananchi hususani huduma afya ili wananchi wasitembe umbali mrefu kufuata huduma za afya badala yake wafanye kazi.

Mpaka kukamilika kwake Kituo cha afya Mikese kitagharimu shilingi milioni mia nne za kitanzania, ambapo kikikamilika kitawasaidia wananchi wa kata ya Mikese na maeneo jilani.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana