Featured

    Featured Posts

NDEGE YA KWANZA YA WATALII YAWASILI LEO UWANJA WA KIA, ZINGINE KUTUA KUANZIA MEI 28


Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema leo majira ya saa 3:30 asubuhi, Ndege ya kwanza iliyobeba watalii ikitokea nchini Ugiriki imetua katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa ni mwanzo wa kurejea kwa usafiri wa anga kwa Ndege za kimataifa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akizungumza na wandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri Kamwelwe amesema Ndege iliyotua leo ilikua na watalii wanne na watu wengine watatu na tayari anayo ratiba ya ndege zingine ambazo nyingi zimeshajaa lakini haswa zitaanza kuja kwa wingi kuanzia Mei 28 mwaka huu.

Amesema kwa upande wa mizigo walianza na Ndege ya Rwanda kwa ajili ya kubeba minofu ya samaki kutokea Mwanza na leo Ndege shirika la Ethiopia itabeba tani 19 za minofu ya Samaki na Jumapili Ndege hiyo itarudi tena Mwanza kubeba tani 40 ya minofu ya samaki.

Amesema uwanja wa Mwanza ambao nao ni wa Kimataifa umeshafunguka kwa ajili ya kubeba mizigo na wanaendelea na mazungumzo na Waziri wa Mifugo ili waweze kusafirisha pia na nyama.

" Wakati huo huo Ndege yetu ya Tanzania tunakamilisha taratibu kadhaa ili nasi tuanze kuruka kupeleka mizigo Ulaya kwa ajili ya biashara.

Niwaombe watanzania tuone fahari kuwa na Nchi nzuri iliyobarikiwa na Mungu na yenye uongozi wenye maono makubwa chini ya Rais Dk John Magufuli, tuungane wote kujenga uchumi wa Nchi yetu na tuchape kazi," Amesema Kamwelwe.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana n ujio wa Ndege za Watalii na kuanza kwa usafiri wa anga.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana