KUNA mnganganyiko mkubwa kwenye matokeo ya vipimo vya sampo za Corona.Ndivyo anavyoelezea Rais Dk.John Magufuli baada ya kufanyika kwa uchunguzi kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama katika Maabara ya Taifa ya Tanzania kuhusu vipimo vya Corona.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli katika maabara hiyo iliyokuwa inapima Corona kuna changamoto nyingi za ajabu hasa baada ya kuona kila wanapotoa matoeo basi lazima yawe Positive, positive tu mara nyingi.
Hivyo alipokuwa akizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama siku za karibuni alivitaka viende kufanya uchunguzi kuhusu vipimo hivyo vikoje na vinafanyaje kazi na kwamba mara nyingi amekuwa akisisitiza sio kila kitu unachopewa lazima kiwe kizuri wanaweza kutumika watu, vinaweza kutumika hivyo vifaa, lakini pia inaweza kuwa ni hujuma kwasababu hii ni vita.
Rais Dk.Magufuli akizungmza leo wakati wa kumuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Mwigulu Nchemba amesema anamshukuru Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mchembe kwani amekwenda na kufanya mambo yafuatayo kwa kutumia vyombo vyetu.
"Tulichukua sampo za Mbuzi , Kondoo, Papai,Oili ya magari na sampo nyingine za vitu mbalimbali na kisha kuvipeleka kwenye maabara ya Taifa kwa ajili ya kuvipima.Tulifanya hivyo bila wao wao kujua na tukazipa majina .
"Sampo ya oil kwa mfano iliyotoka kwenye gari ilipewa jina la Jabir Hamnza(30) , ile ilileta matokeo haina Corona,tulipopeleka sampo ya Fenesi ambalo lilipewa jina la Sarah Samweli(45)matokeo yalionesha kuwa na Corona, tulikopeleka sampo ya Papai na kupewa jina la Elaberth Anne( 26) matokeo yalionesha Papai lina Corona,"amesema Rais Magufuli.
Amefafanua maana yake ni maji ya mle ndani kwenye Papai yana Corona na kuongeza walipeka sampoya ndege Kware matokeo yake naye akawa na Corona, walipeleka sampo ya Mbuzi akawa na Corona , wakapeleka Kondoo akawa hana Corona.
"Sasa tukishaona umepeleka sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ikaleta matokeo ya kuwa na Corona maana yake mapapai yote yangewekwa katantini, ukipelekea sampo ya Mbuzi na ukaambiwa ana Corona maana yake mbuzi zote nazo ziwe karantini.Ukipeleka fenesi likawa positive , hivyo mafenesi nayo yalitakiwa kuwa karantini.
"Ukishagundua kitu kama hiki lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika kwenye vipimo hivyo, kuna mambo ya ajabu yanafanywa katika nchi hii, aidha wahusika wamenunuliwa au hawana utalaam jambo ambalo sio kweli kwani maabara hiyo imekuwa ikitumika sana kwenye magonjwa mengine.
"Aidha zile sampo zilizopelekwa kwasababu kila kitu kinatoka nje, hadi vile vipamba vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa na kama mapapai nayo yanaonekana positive yana Corona basi WHO inatakiwa kufanya kazi kubwa katika hili,"amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kama hali ndivyo ilivyo basi kua uwezekano mkubwa wanasayansi hawajafanya tafiti za kutosha katika hilo, kwa hiyo kuna watu kutokana na mazingira ya aina hiyo huenda wameambiwa wana Corona wakati hawana.
"Inawezekana wengine wakafa kwa hofu wakati Papai lile lipo linaiva, Mbuzi yupo hajafa , Fenesi lipo labda lije lioze tu baadae kwa muda wake.Fenesi lipo kwasababu halisikii huenda lingekuwa linasikia nalo muda huu lingeshaoza.Kwa hiyo natoa mwito kwa Watanzania msiwe na hofu na hasa kwa wale ambao hawajachoka wala kuumia,"amesema Rais Magufuli.
Pia amesema lazima kuwe na maswali mengi ya kujiuliza kama Tanzania, Afrika na Dunia huku akisisitiza huenda kuna kitu fulani hakijafahamika kwa Watanzania, na kwa wanasayansi na inawezekana hata duniani hawajakielewa.Hivyo ametoa mwito kwa wale wanaotumia vifaa hivyo kwa Afrika wachukue sampo za wanyama au hata za kitu chochote hata likuta, mjusi, wachukue chochote , watakuja kuthibitisha hayo anayozungumza.
"Mimi ni mwanasayansi,najua ninachozungumza, na kazi hii imefanywa na watu wenye ujuzi wa hali ya juu.Narudia kuwaambia Watanzania tusipaniki tuendelee kuchapa kazi, uzalishaji uendelee, tusitishane na wanasiasa waache kuchukua hii kama ajenda haitawasaidia
"Mtu anazungumza funga Dar es Salaam, funga Tanga, sifungim nilishasema sifungi na sitafunga.Tuchape kazi na tuendelee kuchukua tahadhari.Sasa wewe kama Waziri wa Katiba na Sheria nenda kashiriane na Wizara ya Afya kuangalia kwenye hiyo maabara kuna nini ndani.
"Kama kuna kitu kama Criminal basi kishughulikiwe kwa mujibu wa sheria, kama kuna watu walijihusisha kufanya Criminal kwa kutumia hivyo vifaa basi sheria ichukue mkondo wake, na kama vifaa hivyo vinatatizo kiufundi basi navyo viangaliwe,"amesema Rais Magufuli.
Post a Comment