Jimbo la Busokelo ni kati ya Majimbo saba ya uchaguzi kwa Mkoa wa Mbeya, lina tarafa moja, Kata 13 ambazo ni Kata ya Mpombo, Kandete, Isange, Luteba, Lwangwa, Kabula, Mpata, Itete, Lufilyo, Lupata, Kisegese, Ntaba na Kambasegela. Na vijiji 56, Matawi ya CCM ni 72.
Kwa kuwa mambo mengi yaliyofanywa na Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Atupele Mwakibete katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichompa ridhaa ya kugombea Ubunge na hatimaye kushinda kuwa Mwakilishi wa wana Busokelo kwa nafasi ya Ubunge, yeye na timu yake wametumia mda wao kutengeneza au kuandika Taarifa ya utekelezaaji huo katika kipindi cha miaka mitatu, kuanzia Novemba 2015 – Novemba 2018, unajulikana kwa umma wa Watanzania hususani Wananchi wa jimbo hilo.
Utekelezaji wake huo, pamoja na kuzingatia mambo muhimu yaliyoainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi, umegusa pia baadhi ya ahadi alizozitoa Rais Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wake Samia Suluhu Hassan Aidha ahadi zote zilizotekelezwa na zile zinazoendelea kutekelezwa zitaonekana katika majedwali katika taarifa hiyo. Kuisoma Taarifa hiyo Tafadhali >> BOFYA HAPA
Post a Comment