Featured

    Featured Posts

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA


Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaQUALITY SPORT IMAGES/GETTY
Image captionPhilippe Coutinho ameshindwa kutamba Barcelona na amepelekwa Bayern kwa mkopo
Klabu ya Newcastle itatumia pauni milioni 70 kumsajili mchezaji wa nafasi ya kiungo wa Barcelona, raia wa Brazil Philippe Coutinho ikiwa pendekezo la klabu hiyo kununuliwa litafanikiwa. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 anaichezea Bayern Munich kwa mkopo. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kampuni ambayo inaelekea kuwa wamiliki wapya wa Newcastle pia inataka kumsajili beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. Mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Italia kwa kitita cha pauni milioni 69.8. (Sky Sports via Star)
Kalidou KoulibalyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHuenda Kalidou Koulibaly akahamia Liverpool kama atapata fursa
Hata hivyo, Koulibaly anafikiria kuhamia Liverpool. (Calciomercato - in Italian)
Mchezaji anayelengwa na Chelsea Dries Mertens bado hajaridhia kuongeza mkataba wake na Napoli . Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Ubelgiji, 33, mkataba wake unamalizika msimu huu. (Calciomercato - in Italian)
England Jadon SanchoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJadon Sancho winga wa England
Borussia Dortmund wanategemea winga wa England Jadon Sancho, 20, kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo, ingawa Manchester United pia imeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo. (Sky Sports)
Winga wa Wolfsburg na Kosovo Milot Rashica,23, anatolewa macho na Liverpool, rais wa shirikisho la soka la Kosovo ameeleza. (Standard)
Mauro IcardiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Paris St-Germain Mauro Icardi
Arsenal wanaweza kupewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 27, ikiwa ni mbadala wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang, 30. Mkataba wa Aubameyang unatarajiwa kumalizika msimu ujao, wakati Icardi anacheza kwa mkopo Paris St-Germain. (Tuttosport via Teamtalk)
Washika bunduki hao pia wako njiani kuingia makubaliano na mchezaji huru George Lewis. Winga huyo wa Norway mwenye miaka 19, alikuwa akiichezea Tromso. (Metro via Goal)
Mchezaji wa miaka 16, wa klabu ya Barcelona Marc Jurado ametupilia mbali ofa kuchezea klabu hiyo ya Uhispania. Beki huyo wa kulia anajiandaa kujiunga na Manchester United.(ESPN)
Sergej Milinkovic-SavicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSergej Milinkovic-Savic (kulia) anayenganganiwa na timu kadhaa
Chelsea, Manchester United na Tottenham wote wanamtaka kiungo wa Lazio, Sergej Milinkovic-Savic. Mchezaji huyo raia wa Serbia, 25, ataruhusiwa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 80. (Mail)
Leeds United wanapendelea kumsajili kiungo wa kati wa Linfield Charlie Allen,17, ambaye pia amewavutia Chelsea, Tottenham na Liverpool. (Yorkshire Post)
Chelsea pia wanavutiwa na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Monaco Fode Ballo Toure, 23, ambaye mkataba wake utakamilika mwaka 2023. (Foot Mercato - in French)
Henrikh MkhitaryanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal inataka kumuuza mchezaji Henrikh Mkhitaryan
Wakala wa Henrikh Mkhitaryan amekana taarifa kuwa Arsenal inampango wa kumuuza mchezaji huyo raia wa Armenia. Mino Raiola amesema tetesi kuhusu kiungo huyo wa kati, 31, ''si za kweli'' (Express)
Kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic,32, amesema hafikirii kuhusu kuihama klabu hiyo pamoja na kuwa mkataba wake utakwisha mwaka 2021.(Sky Germany-in German)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana