Featured

    Featured Posts

TETESI ZA SOKA ULAYA

Pierre-Emerick Aubameyang

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang akifanya mashambulizi katika mechi dhidi ya Burnley
Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, alimuahidi marehemu babu yake kuwa atachezea Real Madrid. (Sun)
Gunners pia wanakabiliwa na pigo jingine la kumkosa beki wa RB Leipzig wa miaka 21-Mfaransa Dayot Upamecano baada ajenti wake kusema kuwa huenda asihame kutokana na janga la coronavirus. (Sport 1, via Metro)
Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, raia wa Nigeria atarejea klabu hiyo baada ya kuchezea Manchester United kwa mkopo kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya China, ambayo imepangiwa kuanza mwezi Julai. (Sky Sports)
Odion IghaloHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionShanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, atarejea klabu hiyo kutoka Manchester United
Huku hayo yakijiri, Manchester United wamefufua azama yao ya kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Sport, via Mail)
Tottenham na Arsenal wameongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa sababu mashauriano ya kiungo huyo wa miaka 31 kurefusha mkataba Chelsea yamegonga mwamba. (football.london)
ChelseaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Chelsea wakisherehekea ufungaji bao
Borussia Dortmund wanataka kumsaini kinda wa Chelsea ambaye anacheza safi ya kati Charlie Webster 16, na kumpandisha hadhi hadi kiwango cha Jadon Sancho. (Sun)
Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amekiri kwamba itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuwapoteza wachezaji wake nyota msimu huu - licha ya tetesi kuwa Chelsea inamnyatia mshambuliaji Ufaransa wa miaka 23-Moussa Dembele. (Star)
Moussa DembeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionChelsea inamnyatia mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele
Baba yake kiungo wa kati wa Brazil Gerson, amedai kuwa Arsenal na Tottenham wanapania kumsaini mchezaji huyo wa miaka 22 kutoka Flamengo. (ESPN, in Portuguese)
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram kumfuatilia Dries Mertens, ripoti zinasema Lampard amewasiliana moja kwa moja na mashambuliaji huyo wa miaka 33- wa Ubelgiji na Napoli. (Express)
Dries MertensHaki miliki ya pichaEPA
Image captionDries MertenSs amefungia Napoli mabao 116
Manchester City inataka kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain Edouard Michut, 17. (Sky Sports)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana