Askari 7 wameuawa katika shambulizi la silaha lililotekelezwa na wanamgambo wa Taliban katika kituo cha jeshi magharibi mwa Afghanistan.
Wizara ya Ulinzi imetangaza kwamba wanamgambo walishambulia kituo cha jeshi katika kijiji cha Akazi wilayani Bala Murgab.
Imeelezwa kuwa askari 7 wamepoteza maisha yao na askari 5 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.
Hata hivyo, inasemekana kuwa Taliban nao wamepoteza idadi kubwa ya wanamgambo wao wakati wa shambulizi hilo.
Post a Comment