Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanapotenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuwapatia mikopo vijana,wanawake na watu wenye walemavu wawape fursa hiyo hasa vijana wanaotaka kuondoka kwenye matumizi ya Dawa za kulevya.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua kituo cha kutoa Tiba ya methadone kwa waratibu wa Dawa za kulevya ambapo Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wamekijenga katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kitakachogharimu zaidi ya Millioni 700 ambacho kitakamilika mwezi wa December mwaka huu.
Post a Comment