TEGETA, Dar es Salaam
Kanisa Halisi la Mungu Baba limeonyesha kuwa miongoni mwa Taasisi za Kijamii ambazo zimeendelea kuunga mkono mwito wa Rais Dk. John Magufuli wa kuwataka Watanzania kuacha hofu dhidi ya Corona, badala yake wachape kazi za kujenga uchumi huku wakiendelea kuchukua thadhari tu dhidi ya ugonjwa huo.
Katika kuonyesha kuunga mkono mwito huo wa Rais, Kanisa hilo limekuwa likihamasisha waumini wake kufanyakazi za uzalishaji kila mmoja katika nafsi yake na kisha kuwakutanisha kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa na kuziuza.
Jumapili iliyopita Kanisa hilo lilifanya maonyesho ya bidhaa na huduma, ambayo licha ya kuyatumia kutangaza bidhaa na huduma lakini waumini waliweza pia kuuza bidhaa zao na kujiptia fedha.
Akihubiria waumini kabla ya kuanza maonyesho hayo, kiongozi wa kanisa hilo Baba wa Uzao alisema ibada ambayo Mungu Baba anapendezwa nayo ni uzalishaji siyo kilio na maombolezo.
"Jamii leo ielewe kuwa Ibada ambayo MUNGU BABA anapendezwa nayo ni Uzalishaji siyo kilio na maombolezo. Tuache ile fikra kuwa Kanisani ni mahali pa wenye shida na matatizo na kusubiri muujiza. Huo ni utumwa ambao tuliingizwa na nyoka ambaye ndiye alibaki na Bustani zote." alisema Baba wa uzao. Kwa Mahubiri kamili ya Ibada hiyo BOFYA HA
Post a Comment