Featured

    Featured Posts

CCM YAWAPONGEZA UVCCM KWA KUENDESHA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JUMUIYA HIYO

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akifanya uizinduzi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoa wa Mbeya, leo.

CCM Blog, Mbeya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Jumuiya yake ya Umoja wa Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kufanikisha uendeshaji wa Mradi wa ujnezi wa nyumba  za watumishi wa Jumuiya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole wakati wa uzinduzi wa nyumba za makatibu wa UVCCM akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake katika mkoa wa Mbeya. 

Katika hafla hiyo, Polepole amezindua ujenzi wa  nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbeya na nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya ambazo zinajengwa kwa michango ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi tu.

"Nawapongeza sana wana CCM na UVCCM kwa jumla kwa Umoja wenu uliyofanikisha ujenzi wa nyumba hizi", amesema  Polepole wakati akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Polepole ametumia hafla hiyo ya uzinduzi wa nyumba hizo kuchangisha papo hapo ya Ujenzi wa nyumba hizo na kufanikisha kupatikana sh. milioni 10 zikiwemo fedha taslimu na ahadi.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka Polepole amewataka wana CCM kuwa wamoja na kuchagua Viongozi wanaokubalika kwa Wananchi akifafanua kwamba katika Uchaguzi huo ndani ya Chama, CCM itasimamia katiba, kanuni na taratibu zake nzuri ili kuhakisha inapata Viongozi hao wanaokubalika ndani ya Chama na kwenye umma. PICHA ZAIDI>>BOFYA HAPA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana