Akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika eneo la Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoani Mwanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Humphrey Polepole ambaye pia ni Mlezi wa vijana wa CCM wanaosoma vyuo na vyuo vikuu, amewataka vijana kuendelea kuwa wazalendo, kutambua na kuisemea kazi nzuri ambayo imefanyika katika Uongozi wa Awamu ya Tano Chini ya Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameyasema hayo Katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) alipokuwa amealikwa kutoa mhadhara uliokuwa na mada inayosema mazingira ya kisiasa ya Tanzania na namna yanaweza kuathiri biashara na masoko kimataifa
Ndg. Polepole amesema kati ya mambo makubwa ambayo yamefanyika na Uongozi wa Rais Magufuli ni kukipigania Kiswahili ili kitambulike kama lugha rasmi katika Umoja wa Afrika na Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na kwamba kwa ushawishi wa Rais Magufuli kwa Marais wenzake wa Afrika amewezesha kukuza biashara kati ya nchi hizo baada ya kuanza kutumika kwa Kiswahili kama lugha ya rasmi ya mawasiliano katika nchi za Afrika
Post a Comment