Featured

    Featured Posts

DUNIANI KUNA MAMBO: TOKYO NCHINI JAPAN KILA MWAKA HUFANYA SHEREHE YA KUJIANDAA NA KIFO

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
UNAHISI vipi ukiambiwa kuhusu kifo? ni wazi kuwa wengi hawafurahii kusikia habari hizo, lakini watu wengi kutoka Tokyo nchini Japan wanafurahi wakisikia habari kuhusiana na kifo, watakufa vipi? na namna ya kujiandaa kabla ya kifo.

Tokyo hufanya sherehe kila mwaka kwa ajili ya kujiandaa na kifo, "Shukatsu Festival" watu hufundishwa namna ya kujiandaa kwa kifo, "Shakatsu" kwa wajapani humaanisha kujiandaa kabla ya kufa na maadhimisho hayo hufanyika kila Desemba 16.

katika maadhimisho hayo watu hujengewa uelewa wa namna watakavyowaacha wapendwa wao wakipitiwa na kifo, maadhimisho hayo huambatana na maonesho mbalimbali yanayohusu kifo na kwa kuweka uhalisia zaidi   watu hulala katika majeneza, wakiwa wamevaa mavazi ya marehemu huku mafunzo ya namna ya kuanda miili ya wafu yakiendelea.

Wengi walioshiriki sherehe hizo wamekuwa wakieleza kuwa wanataka kuona mwisho wao kabla ya kuufikia na wengi wao hulala katika majeneza na kupiga picha na baadaye huchagua mapambo, maua na kila kitu ambacho wangependa kitumike katika siku zao za mwisho.

Japan si nchi yenye watu wengi duniani (watu milioni 126.5 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018) bali pia ni moja ya nchi ambayo inaongoza kwa kuwa kampuni nyingi za mazishi na kumekuwa na washiriki wa kada zote wakiwemo wazee na vijana katika sherehe hizo.

Imeelezwa kuwa maonesho hayo yamelenga kuwakumbusha watu kuhusiana na kifo pamoja na majonzi na huzuni kwa wale wanaoachwa na imeelezwa kuwa maonesho hayo yamekuwa ni mwongozo bora katika familia hasa kwa kuzingatia safari ya kifo.

Sherehe hizo zimekuwa zikiwavuta pia watalii kutoka nje huku kapuni za mazishi nchini humo zikipata wateja wengi kupitia Shukatsu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana