Featured

    Featured Posts

IGP SIRRO AFANYA UHAMISHO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime imesema, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amefanya uhamisho kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa ili kuongeza ufanisi na tija katika kazi za Polisi. 

Miongoni mwa waliohamishwa, amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu namba moja  katika Shule ya Polisi Moshi.

Pia IGP Sirro, amemhamisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Bunge, Dodoma ACP Emmanuel Lukula kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na nafasi yake inachukuliwa na ACP Andrew Satta ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana