Mchezaji wa Tottenham aliyesaini kandarasi iliovunja rekodi ya dau la £54m Tanguy Ndombele, 23, amemwambia mkufunzi wake Jose Mourinho kwamba hataki tena kucheza chini yake. Paris St-Germain, Barcelona na Bayern Munich zote zinamnyatia kiungo huyo wa kati wa Ufaransa. (ESPN)
Barcelona itavutiwa na mpango wa kubadilishana wachezaji huku Ndombele akijiunga na timu hiyo na winga wa kulia wa Portugal Nelson Semedo, 26, au winga wa Brazil Phillipe Coutinho 28 ambaye kwa sasa yuko Bayern Munich kwa mkopo akijiunga na Spurs. (Independent)
Juventus imeulizia kuhusu mashambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre- Emerick Aubameyang, 31, ikijiunga na Bareclona na Intermilan miongoni mwa timu zilizovutiwa na mchezaji huyo.(Le10 Sport - in French)
Beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29, anatarajiwa kujiunga na Manchester City mwisho wa msimu huu baada ya Liverpool kutafuta mchezaji mwengine. (Express)
Kiungo wa kati wa Brazil Fred, 27, anataka kusaini kandarasi mpya katika klabu ya Manchester United. (Sun)
Manchester United ndio chaguo la winga wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 20. Lakini klabu hiyo ya Bundesliga haitamuachilia kwa chini ya £118m. (Bild - in German)
Liverpool wanapigiwa upatu kumsaini Thiago Alcantara kwa dau la £43m baada ya kiungo huyo wa Uhispania, 29, kuvunja mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake Bayern Munich. (Bild - in German)
Everton, Tottenham na Wolves zinataka kumsaini beki wa Paris St-Germain na Brazil Thiago Silva. Mchezaji huyo mwennye umri wa miaka 35 ameripotiwa kutaka kuhamia England. (Goal - in Portuguese)
Arsenal imewasiliana na klabu ya Sporting Lisbon kuhusu uhamisho wa kinda wa Portugal Joelson Fernandes, 17. Hatahivyo , mshambuliaji huyo anazivutia klabu kama Barcelona na RB Leipzig. (O Jogo via Star)
Mkufunzi wa klabu ya Saint-Etienne Claude Puel anataka kuongeza kandarasi ya mkopo ya beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba hadi baada ya fainali ya kombe la Coupe de France. (Goal)
Kiungo wa kati wa Chelsea na England Mason Mount, 21, amewanunulia tiketi za klabu ya Vitesse Arnhem wafanya kazi wa afya wasio na uwezo wa kununua tiketi hizo baada ya kuhudumu kwa mkopo katika klabu hiyo msimu wa 2017-18. (Mail)
Norwich inajianda kumsaini kiungo wa kati wa Sunderland na England Bali Mumba, 18, katika mkataba utakaogharimu £350,000. (Sky Sports)
Post a Comment