Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchiu Eng. Mhe. Hamad Masauni akiwa na mkoba ukiwa na Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg Galos Nyimbo, Hafla hiyo imefanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na mkewe Thania Abdulla(kulia) wakati akiwasili Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM),kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Katibu wa Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg Galos Nyimbo akikabidhi fomu za kujaza wafamini wake Mgombe Urais wa Zanzibar Eng. Mhe. Hamad Masauni wakati wa hafla ya kuchukua Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar.
Katibu wa Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Kada ya CCM Eng. Mhe. Hamad Masauni, wakati wa zoezi la kukabidhiwa fomu katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Eng. Hamad Masauni akiwa na Mkewe wakitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar baada ya kumaliza zoezi la kuchukua fomu ya Urais wa Zanzibar na kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari Zanzibar.
Post a Comment