Featured

    Featured Posts

WAZIRI WA KILIMO ZANZIBAR, MMANGA MJENGO MJAWIRI AJITOSA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

Kada wa Chama Cha Mapinduzi Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akichukua Fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM, akikabidhiwa na Katibu Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.  
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg.Galos Nyimbo akimkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri alipofika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar kuchukua fomu ya Urais.
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua baada ya kukamilika zoezi la kukabidhiuwa Fomu ya Urais, akielekea katika viwanja vya Kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwa ajili ya kuomba dua baada ya kukabidhiwa fomu ya Urais kupata baraka za Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar CCM Mhe.Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akiomba dua katika kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume baada ya kukamiulisha zoezi la kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar.

Kada wa CCM Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika viwanja vya Afisi Kuu Kisiwandui Zanzibar kushuhudia Wananachama wa CCM wanaojitokeza kuchukua Fomu ya Urais.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana