Featured

    Featured Posts

RAIS MAGUFULI NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU AMBAYO TUMEPEWA WATANZANIA-MBUNGE CCM


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Amina Mollel (CCM) amelieleza Bunge kuwa Rais Dkt.John Magufuli ni zawadi tuliyopewa na Mungu, hivyo kikubwa ni kuendelea kumuombea awe na maisha marefu zaidi.

Mollel amesema hayo wakati wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Bungeni Mjini Dodoma ambapo wabunge walipata nafasi ya kujadili maazimio mawili, Azimio la kwanza ni kumpongeza Rais Magufuli na azimio la pili ni kumpongeza Spika wa Bunge Job Ndugai.

Akieleza zaidi mbele ya wabunge Mbunge Mollel amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akitamka hapo bungeni kuwa Rais Magufuli ni zawadi ya watanzana kutoka kwa Mungu.

"Ni zawadi kwasababu ni Rais mwenye ujasiri, uthubutu, muongoza njia ambaye amekua akituongoza kuelekea uchumi wa kati.Tunajivunia kuwa na Rais Magufuli, tunajivunia kuwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, tunajivunia kuwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, tunajivunia kuwa na Baraza la Mawaziri ambalo limekuwa likimsaidia Rais kwa ukaribu zaidi katika kulipeleka taifa katika maendeleo.

"Katika mafanikio makubwa ambayo Rais Magufuli ameyafanya ni kutokana na uwepo wa wasaidizi wake ambao nao naomba niwapongeze. Nakumbuka tumekuwa tukisikia Serikali kuhamia Dodoma lakini sasa tunashuhudia chini ya Rais Magufuli Serikali imeshahamia Dodoma.

"Baada ya kupitishwa azimio hili ambalo tunalijadili hapa naamini hakutakuwa na mtu mwenye maono mengine ya kuiondoa Serikali hapa Dodoma. Haya ni maajabu ambayo yanafanywa na Rais Magufuli, amekuwa Rais wa mfano na Dodoma ambayo inaonekana leo hii baada ya miaka 10 ijayo itakuwa tofauti kabisa na hata wale ambao waliondoka hapo nyuma wakirudi leo watashangaa,"amesema Mollel.

Ameongeza kikubwa ambacho Watanzania wanatakiwa kukifanya ni kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Rais Magufuli ili azidi kuwa na afya njema na maisha marefu zaidi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana