Featured

    Featured Posts

WABUNGE WAPITISHA AZIMIO KUMPONGEZA DK.MAGUFULI, SPIKA JOB NDUGAI KWA KULIONGOZA VEMA BUNGE LA 11

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja wamepiga kura ya kupitisha Azimio la kumpongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kufanikisha shughuli za Serikali kuhamia Dodoma ambapo wamekubaliana hakutakuwa na mtu mwingine yoyote anayeweza kuja kuiondoa Serikali na shughuli zake Dodoma.

Wakati Azimio la pili ambalo wabunge wamelipitisha linahusu kumpongezi kwa Spika wa Bunge Job Ndugai kutokana na mafanikio ambayo yamepatikana kwenye Bunge la 11kutokana na uongozi wake mahiri.

Naibu Spika Dk.Tulia Ackson wakati anazungumza mbele ya wabunge leo Juni 8 mwaka 2020, amesema anawashukuru wabunge wote kwa jinsi ambavyo wamechangia maazimio yote mawili na kura ambazo zimepigwa wabunge wengi wameunga mkono na wapande zote.

"Wabunge wote wakiwemo wa upande wa pili wamepitisha maazimio yote mawili.Hivyo niwatoe hofu hata wale waliokuwa wanaonekana kutounga mkono kwenye majadiliano wamepiga kura na kuunga mkono,"amesema Dk.Tulia.

Awali wabunge mbalimbali wamepata nafasi ya kumuelezea Spika Ndugai kwa jinsi ambavyo ameliongoza vema Bunge la 11 na kuwa la mafanikio makubwa huku wakisifu alivyofanikisha teknolojia kutumika katika kufanikisha shughuli za Bunge.

Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga ametumia nafasi hiyo kumuelezea Spika Ndugai kuwa ni Spika mwenye maoni makubwa yanayokwenda sambamba na maono ya Rais Dk.Magufuli.

Kitwanga amesema uongozi wa Spika Ndugai katika Bunge la 11 umeacha alama itakayochukua miaka mingi bila kufutika na hasa ya namna alivyofanikiwa kutengeneza mifumo ya kudumu na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za Bunge.

"Katika kuongoza nchi kuna maoni ya mbali.Hoja hii ya kumpongeza Spika inaonesha namna ambavyo amemuelewa Rais wetu ili kufikia maono yake.Hatuzungumzii Spika kwa mawazo madogo, Spika ambacho amekifanya ni kujenga system, hivyo awe yupo au ameondoka mfumo ambao ameuweka utabaki.Mtu mwenye maono ya namna hii anastahili pongezi,"amesema.

Hata hivyo Kitwanga wakati anamuelezea Spika Ndugai amesema leo amethibitisha uwepo wa wabunge wenye akili ndogo na wenye akili kubwa huku akitumia nafasi hiyo Watazania mama yetu ni Tanzania , baba yetu ni Mungu na Rais wetu ni Dk.John Magufuli.

Awali Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Mkamia wakati anamulezea Spika Ndugai amesema kama binadamu atakuwa na mapungufu yake lakini kama Spika wa Bunge amekuwa kiongozi ambaye ameweza kulisimamia Bunge hilo kwa ufanisi mkubwa na pongezi anazopewa na wabunge anastahili.

Wabunge wengine weamua kutoa ya moyoni kuhusu Spika Ndugai kwa kueleza wazi, mbali ya kuongoza vema Bunge, ni Spika ambaye ana upendo mkubwa kwa wabunge wenzake na amekuwa akitatua changamoto za wabunge mbalimbali hata zile changamoto za kifamilia.

Pia wamesema Spika Ndugai ameonesha ujasiri mkubwa wakati wa janga la Corona kwani aliamua kusimamia Bunge kuhakikisha linaendelea na shughuli zake na hasa kwa kutambua wajibu wa Bunge kwa maendeleo ya Watanzania na nchi yetu.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana