Shirika la Viwaango Tanzania (TBS) litaanza kutumia maabara ya uvuvi ya Nyegezi Mwanza (National Fish Quality Control Laboratory-NFQCL) katika upimaji wa sampuli za chakula zinazochukuliwa kwenye viwanda na masoko.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt Athuman Ngenya ameyasema hayo leo wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa WIizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe aliyeambatana na Naibu wake Mhe. Ludovick Nduhiye, katika ofisi za TBS jijini Mwanza.
Dkt. Ngenya amesema kwa sasa TBS na NQCL zipo katika hatua ya mwisho ya maridhiano kwa ajili ya ofisi za TBS Kanda mutumia maabara hiyo kwa ajili ya upimaji wa sampuli za chakula zinazochukuliwa katika kanda
hiyo.
Dkt Ngenya amesema hatua hii itasaidia kutatua changamoto ya ucheleweshaji wa majibu ya maabara na maamuzi juu ya ubora wa bidhaa za chakula hasa zile zilizo na muda mfupi wa matumizi
Post a Comment