CCM Blog, Dar es Salaam
Klabu ya Soka ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imeibuka kidedea baada ya kuichapa Yanga 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyorindima katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
Katika mpambano huo uliokuwa wa kupimana nguvu kujiandaa na mechi za ligi kuu, mabao ya KMC yamewekwa kimiani na Sadala Lipangile katika dakika ya 31 huku Charles Ilafya akifunga bao la pili katika Dakika ya 45, na hadi kuingia kipindi cha pili timu hiyo ilikuwa inaongoza kwa bao 2-0.
Goli la tatu lilifungwa na Hasan Kabunda Dk.65 na kufanya ubao kusomeka 3-0. Hadi kipyenga cha mwamuzi kupulizwa kumalizika kwa mechi ubao ulisomeka KMC 3 YANGA 0.
Post a Comment