Na Scolastica Msewa, Bagamoyo.
Makada 76 wa CCM wamechukua fomu za kuwania kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii ofisini kwake katibu wa CCM wilaya ya bagamoyo Getruda Bonifasi Sinyinza amesema idadi hiyo ni hadi kufikia saa 10 jioni siku ya tarehe 17 wakati wa kuhitimisha zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu rasmi nchini kote ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Getruda amesema wilaya ya Bagamoyo ina majimbo ya uchaguzi mawili yaani jimbo la Bagamoyo na jimbo la Chalinze ambapo jimbo la Bagamoyo wanaCCM 50 wamejitokeza kuchukua fomu na wanaCCM 26 wakati waliorudisha fomu hizo bagamoyo ni 48 na Chalinze ni 25.
Naye Katibu wa UWT wilaya ya bagamoyo Hanipha Checheta amesema tangu tarehe 14 hadi tarehe 17 saa 10 jioni waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea Udiwani Viti maalumu ni wanawake 44 ambapo waliorejesha ni 42.
Aidha amewashukuru wanawake hao kwa moyo wa kuthubutu ili kugombea kwani matarajio yalikuwa wanawake zaidi ya 100 wangejitokeza kuwania Udiwani Viti maalumu wilayani Bagamoyo.
++++
Katimu Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo ambaye ni Katibu wa UVCCM wa Japhet Thobias wilaya hiyo akipokea fomu kutoka Gadi Lameck Kalibwani aliyekuwa anarejesha fomu ya kuwania jimbo la Bagamoyo.
Katimu Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo ambaye ni Katibu wa UVCCM wa Japhet Thobias wilaya hiyo akipokea fomu kutoka kwa Boniphace Magaesa aliyekuwa anarejesha fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Bagamoyo
Katimu Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo ambaye ni Katibu wa UVCCM wa Japhet Thobias wilaya hiyo akipokea fomu kutoka kwa mbunge wa zamani wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa aliyekuwa anarejesha fomu ya kuwania tena jimbo hilo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Chalinze Ayubu Kikando Kastam wakati wa mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Bagamoyo Abbas Amri Kiombya wakati wa mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu.
Post a Comment