Featured

    Featured Posts

MWENYEKITI WA CCM BAGAMOYO ATAJA SABABU YA WENGI KUHAMASIKA KUWANIA UBUNGE. UDIWANI KWA TIKETI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Alhaji Abdul Sharif Zahoro akizungumza ofisini kwake.

Na Scolastica Msewa, Bagamoyo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Alhaji Abdul Sharifu Zahoro amesema utendaji bora wa Chama na uwazi wa chama kuanzia ngazi ya taifa ni moja ya hamasa kubwa kwa wanaCCM wengi kuchukua fomu za kugombea ngazi ya ubunge na udiwani.

Amesema hayo mjini Bagamoyo Ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari Sharifu amesema kuanzia Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli amekuwa akitekeleza kwa vitendo kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mmoja ndani ya chama.

Amesema idadi ya waliojitokeza kuchukua fomu ni kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu dunia ilipoumbwa lakini katika awamu hii imetokea.

Ameongeza kuwa hii ni kutokana na wananchi na wanaCCM kuwa na imani na Chama na safu za uteuzi zilizopo.

Hata hivyo Sharifu amesema uongozi wa CCM wilaya umejipanga kuhakikisha kila aliyechukua fomu ya kugombea anatendewa haki kwani uchaguzi utakuwa wa wazi kama ilivyokuwa katika uchaguzi mkuu wa CCM taifa.

“kwamba baada ya kura kupigwa zitahesabiwa pale pale na matokeo yatatangazwa hapo hapo na kila mtu atapewa kura yake ili kuondosha maneno maneno kwa baadhi ya watu kusema kura zimeibiwa au ulete wakala wakusaidia kuhesabu kura hakuna hiyo kwani kila mgombea atashika kura yake ataihesabu mwenyewe ili hatimaye tujue nani ameongoza” alisema Sharifu.

Aidha ameungana na mwenyekiti wa CCM taifa kuwataadharisha wanaCCM na wananachi kuwa baada ya kuchukua fomu na kuruidisha wasifanye kampeni wala wasitoe rushwa kwani Chama kimekataza wagombea kutoa Rushwa.

“Uongozi anatoa Mwenyezi Mungu hivyo ni ili kupata nafasi husika lazima uendane na kanuni na maadili ya chama na taratibu za Nchi kwani TAKUKURU wamejipanga vizuri sana na Yeyote atakayedhibitika kutoa na kupokea rushwa fomu yake haita jadiliwa” alisema Sharifu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana