Chama Cha Mapinduzi kimeeleza matokeo na mafanikio ya Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli kuwekeza katika elimu iletayo ukombozi ikiwa ni pamoja na utolewaji wa elimu bure shule ya msingi mpaka sekondari, majaribio ya utolewaji wa elimu bila malipo kwa mafunzo ya ufundi stadi sambamba na mikopo ya elimu ya juu.
Uwekezaji mkubwa katika elimu umewezesha wananchi kuzibaini fursa za kujiletea maendeleo kwa haraka zaidi na kuwasogeza karibu na serikali na sekta binafsi katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
Akiyasema hayo Leo, katika mdahalo wa Uzalendo ulioandaliwa na Jukwaa la waalimu wazalendo Mkoa wa Mbeya, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole ameeleza ni Elimu ya Ukombozi ndio imewezesha kutambua uonevu uliokuwa ukiendelea kwenye Madini na maeneo Mengine, na ni Elimu hii ndio imepelekea Serikali ya Awamu ya Tano kuwekeza katika Miradi Mikubwa ya Kimkakati iliyolenga kumkomboa Mtanzania mnyonge mapema Zaidi kuliko ilivyo tarajiwa.
Ndugu Polepole ameendelea kutoa Rai kwa umma wa watanzania kuendelea kuwa wazalendo na wenye mapenzi makubwa kwa Serikali na Nchi ya Tanzania kwa kuendelea kupigania, Kutetea, na kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Imetolewa na;
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
Post a Comment