Flora Williamu Mrema (pichani), ni kada kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amejitosa kutia nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge jimbo la Moshi la Moshi Vijijini, Tafadhali zisome sifa zake hapa chini baada ya maelezo haya.
WASIFU BINAFSI (CV)
Bi; FLORA WILLIAMU MREMA
MAELEZO BINAFSI
JINA: FLORA WILLIAMU MREMA
TAREHE YA KUZALIWA: 12/01/1988
MAHALI NILIPOZALIWA:
WILAYA: MOSHI VIJIJINI
KATA: MBOKOMU
KIJIJI: KORINI KUSINI
UTAIFA: MTANZANIA
HISTORIA YA KIELIMU
2015-2018: Astashahada ya uzamili ya sheria(Mafunzo ya sheria kwa vitendo) katika chuo cha sheria kwa vitendo Dar Es Salaam(The law school of Tanzania) (L.S.T)
2010-2013: Shahada ya kwanza ya sheria chuo kikuu Tumaini Makumira (TUMA)
2008-2010: Elimu ya sekondari (Advanced level) shule ya sekondari Pasua.
2002-2006: Elimu ya Sekondari (Ordinary level) shule ya sekondari Natiro.
1996-2002: Elimu ya msingi,shule ya msingi Mbokomu- Wilaya ya Moshi vijijini.
UZOEFU WA KAZI NDANI NA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Kamati ya ushindi mwaka 2015 ya mbunge wa Urambo
Nimetetea maslahi ya chama na kukilinda.
Nimeshiriki katika kutetea maslahi ya chama na kuleta amani pale mgogoro unapoinuka ndani au dhidi ya chama.
Nilishiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa jimbo la Moshi vijijini 2019 kuhakikisha viongozi bora wanapatikana.
Nimeshiriki kikamilifu kutoa semina mbalimbali kuhusu sheria za mirathi, sheria za ardhi ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima.
Post a Comment