Featured

    Featured Posts

JOHN CHEYO ANOGEWA NA UTENDAJI WA DK. MAGUFULI, ATANGAZA UPD KUMUUNGA MKONO URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA MWAKA HUU

Mwenyekiti wa Chama United Democratic Party (UDP) John Cheyo akizungumza katika Ofisi za Chama hicho jijini Dar es Salaam, leo.

CCM Blog, Dar es Salaam
CHAMA cha upinzani hapa nchini cha United Democratic Party, (UDP) leo Julai 2, 2020, kimefungua dirisha la uchukuaji fomu kwa wanachama wake wanaotaka kugombea Ubunge na Udiwani, huku kikitangaza kuwa hakitaweka mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa akufanyika Oktoba mwaka, badala yake kitamuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampitisha kuwa mgombea wake wa urais

Mwenyekiti wa Chama UDP John Cheyo (Mapesa) amesema kipaumbele cha Rais Magufuli kuwainua wanyonge na kuleta maendeleo nchini ndio sababu iliyowafanya kuumuunga mkono katika ngazi ya kiti cha Urais, badala ya kuweka mgombea ambaye atampunguzia kura bila sababu.

"Namsifu Magufuli kwa kuboresha uchumi wa nchi kwa kuboresha miundombinu ya usari na usafirishaji wa anga, reli, barabara, bandari na pia kuwabana watumiaji vibaya wa madaraka na arasilimali za nchi tena ameboresha huduma za kijamii kama afya na elimu, ndiyo maana tumeamua kumuunga mkono endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema Cheyo.

Chama cha UDP kimekuwa cha pili kuunga mkono Rais Magufuli baada ya kutanguliwa na Chama Cha TLP ambacho tayari kimeshatangaza pia kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.

Kuhusu kufundua dirisha la wagombea wa Ubunge na Udiwani kupitia UDP, Cheyo amesema  baada ya dirisha hilo kufunguliwa leo, siku ya mwisho wa uchukuaji wa fomu hizo watatangaza kuendana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusema "Natoa Rai kwa wanachama wa UDP, kuja kuchukua fomu ili kuweza kupata nafasi ya  kuingia katika baraza la maamuzi,".
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana