Wizara ya Afya ya nchi hiyo jana usiku ilitangaza kuwa idadi ya watu walioambukizwa corona huko Brazil imefika milioni moja laki sita elfu tatu na 55 baada ya kusajiliwa kesi mpya elfu 26 na 51 za maambukizi ya corona katika masaa 24 yaliyopita.
Wizara ya Afya ya Brazil imeongeza kuwa watu 64 elfu na 867 wameaga dunia pia nchini humo kwa corona; idadi ambayo inaashiria ongezeko la watu 602 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa juzi Jumamosi.
Brazil inashika nafasi ya pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona na pia wale walioaga dunia kwa maradhi ya Covid-19 ikitanguliwa na Marekani.
Ripoti zinasema kuwa hospitali nchini Brazil zinakabiliwa na matatizo chungunzima ikiwemo uchache wa vifaa tiba na kushindwa kulaza wagonjwa wapya.
Post a Comment