Featured

    Featured Posts

RAIS WA GHANA AJIWEKA KARANTINI BAADA YA MPAMBE WAKE KUAMBUKIZWA CORONA

  Rais Nana Dankwa Akufo-Addo wa Ghana amejiweka karantini baada ya mpambe wake wa karibu kuthibitika kuwa ameambukizwa ugonjwa wa COVID-19.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari wa Ghana, Kojo Oppong-Nkrumah imethibitisha habari hizo na kufafanua kuwa, Rais Akufo-Addo amefanya uamuzi huo wa kujitenga kwa muda wa siku 14 kama hatua ya tahadhari inayoendana na protokali za kiafya za kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza.
Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa vipimo alivyofanyiwa rais huyo vimeonyesha kuwa hajaambukizwa virusi vya corona na kwamba katika kipidi hiki cha karantini, atafanyia kazi zake za kiofisi katika Ikulu ya Jubilee.
Mwezi uliopita wa Juni, Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana alitangaza kuwa, Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Kwaku Agyeman Manu amepatwa na ugonjwa wa COVID-19.
Waziri wa Afya wa Ghana aliyekumbwa na corona
Maambukizo mapya ya corona yaliyotangazwa jana Jumapili yameifanya Ghana kuwa na jumla ya watu 20,085  wenye virusi vya corona tangu mripuko wa janga hilo lililoikumba dunia nzima, ulipotangazwa nchini humo kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Machi.
Hadi sasa watu 122 wamefariki dunia kwa maradhi ya COVID-19 nchini humo, huku wagonjwa wa corona waliopata afueni wakiwa ni 14, 870.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana