NAIBU KATIBU WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA ATEMBELEA MAHAKAMA KUU KIGOMA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju (kulia) leo ametembelea Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma ili kujionea hali ya utoaji huduma ya haki kwa wananchi hususan wanyonge, ikiwemo ya Msaada wa Kisheria kabla ya uzinduzi wa Kamati ya Uratibu wa Huduma ya Msaada wa Kisheria Mkoa wa Kigoma. Katika ziara hiyo Mpanju amefanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta (kushoto) ambaye alimwelezea ubora wa huduma inayotolewa katika Mahakama hiyo kupitia Mahakama Mtandao na kuhusu kutoa ofisi kutoka jengo hilo kwa ajili ya huduma ya msaada wa kisheria. (Picha na Festor Sanga- Mahakam, Kigoma)
Post a Comment